Thursday, November 15, 2012

WASOMALI NA WAHABESHI TOKA ETHIOPIA WANAOKAMATWA KILA MWAKA MWAKA MWAMBAO WA ZIWA NYASA NI MRADI WA WATU NA WANANFAHAMIKA

WAHABESHI zaidi ya 98 kutoka Ethiopia wamekamatwa jana katika kijiji cha Ilela Manda mwambao wa ziwa Nyasa katika wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe inasemekana wengine walifanikiwa kutoroka. Lakini hii ni mara ya tatu kukamatwa maeneo hayo ambapo awali walikamatwa wakapelekwa mahakamani na mahakama kutoa amri ya kulipa faini na kuondoka nchini ndani ya siku saba hatujui kama waliondoka au walifichwa na wenyeji.mara ya pili mwaka jana wakakamatwa wasomali 71 katika maeneo hayohayo safari hii walihukumiwa kulipa faini kila mmoja shingi elfu na kurudishwa kwao kwa gharama ya serikali.Novemba 13 wamekamatwa wengine mpaka ninapoandika wako mahabusu Ludewa. naomba ushauri wenu mradi huu ni wa nani? polisi wapo, mahakama zipo. Uhamiaji wapo wanasubiri mishahara. Lakini jambo la kushangaza kuna watu ambao wamekuwa wakiwalipia faini mahakamani tena fedha nyingi. Jamani mnauza nchi. safari nyingine mimi nitawataja kwa sababu wanafahamika na kila mtu.kwani huu siyo uungwana hata kidogo.

No comments:

Post a Comment