Friday, August 9, 2013

PETS YAPIGA HODI LUDEWA, WANANCHI WASEMA TUMETESWA MIAKA 50. Na Bazil Makungu WANANCHI katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wameupokea kwa shangwe na kupongeza Balaza la maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kufikisha mfumo wa ufuatiliaji wa rasrimali za umma(PETS) ambao utasimamiwa na jamii yenyewe katika vijiji vyao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa vijiji vya Luana, Mbwila, Lifua na Kipangala katika kata ya Luilo ambao walishiriki kwa mara ya kwanza kuunda kamati za PETS katika maeneo yao walisema kuchelewa kwa mfumo huu ndiko kumefanya wao kuteswa na watoa maamuzi kwa kuendesha miradi ya serikali kwa kuzingatia maslahi binafsi huki wao wakiendelea kuwa maskini na kupata huduma zilizopo chini ya kiwango.

 Kamati ya Pets ya kijiji cha Luana wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa Pets kutoka Balaza la maaskofu katoliki Tanzania TEC waliokaa kushoto ni Dismasi Sambala mratibu wa Pets baraza la maaskofu,diwani wa kata ya Luana na makamu wa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Tomaso Haule na mratibu wa Pets wilaya ya Ludewa mzee Nkwera.






 Kamati ya Pets kijiji cha Lifua katika kata ya Luilo wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Matei Kongo
 Kamati ya Pets ya kijiji cha Kipangala ikiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa Pets
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Matei Kongo akitoa neno la shukrani kwa wawezeshaji na kuwataka wananchi wa kijiji cha Lifua kuanza kuufanyia Pets mradi wa maji uliopo katika kijiji chao.

No comments:

Post a Comment