Na
Bazil Makungu Ludewa
WANANCHI
Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wamepongeza hatua ya uongozi wa
Benki ya Wananchi njombe (NJOCOBA) kuanza kutoa huduma za kibenki
mjini Ludewa na kuuutaka uongozi wa benki hiyo kuharakisha huduma ya
ATM ili kurahisisha kero ya wateja kwenda kuchukua fedha ndani ya
jengo hasa muda ambao benki inakuwa imefungwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema ujio wa benki hiyo ni
ukombozi kwao kwani katika kipindi chote cha miaka hamsini ya uhuru
Ludewa imekuwa ikitegemea benki moja tu ya NMB jambo ambalo limekuwa
na usumbufu mkubwa.
Meneja
wa benki hiyo tawi la Ludewa Felix Kapinga alisema tawi lake
lilianzishwa julai mwaka huu na kwamba amekuwa akipokea wateja kila
kunapokucha na hii nikutokana na benki yake kujali sana wananchi
lakini kubwa likiwa kuwashirikisha kumiliki benki kwa njia ya kununua
hisa.
‘’’’ tunazo
akaunti za aina mbalimbali ikiwemo akaunti za watu binafsi, akaunti
za watoto,akaunti za pamoja, akaunti za saccos, akaunti za
wafanyabiashara,akaunti za makampuni na akaunti za muda maalum.’’’
aliongeza kapinga
Nani
mwenye sifa ya kununua hisa za Njocoba? ni mtu yeyote wa umri wowote,
kwa makampuni, asasi, taasisi, misikiti, makanisa, vijiji, serikali
na vikundi dhamira ikiwa nikutumia rasrimali zilizopo kwa ajili ya
kuinua hali za maisha kwa wananchi wa kima cha chini, wafanyabiashara
wadogo na wa kati, wafanyakazi, wafugaji na wakulima kwa kutoa huduma
bora za kifedha zinazoendana na mazingira yao.
Kapinga
alizitaja faida za kununua hisa kuwa ni pamoja na kupata gawio la
faida kila mwaka benki inapotengeneza faida, kuwa mmoja wa wamiliki
wa benki, kushiriki mkutano mkuu wa wanahisa kila mwaka na kutoa
mchango wa mawazo kwa ajili ya maendeleo ya benki, kupata faida
itokanayo na ongezeko la thamani ya hisa na kutumia hisa kama dhamana
ya mikopo.
mwisho

No comments:
Post a Comment