Na Bazil
Makungu Ludewa
WAKATI Serikali ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania ikijipanga kuhakikisha wakulima kote nchini wanapata pembejeo kwa
wakati muafaka na kuondoa ukilitimba uliojitokeza katika ugawaji wa vocha za
pembejeo katika msimu wa kilimo wa mwaka jana maafisa watendaji wawili pamoja na
wakala wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kuhujumu uchumi.
Maafisa watendaji waliofikishwa katika
mahakama ya wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ni pamoja na Ayoub Gowele afisa
mtendaji kijiji cha Liugai katika kata ya Luilo, Isaack Haule kaimu afisa mtendaji
kata ya Luilo, Lucas Hinjuson mwenyekiti wa pembejeo kijiji cha Liugai na Moses
Mtewele wakala wa pembejeo wilayani Ludewa.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu
mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna mwendesha
mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Imani Nitume aliiambia
mahakama hiyo kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo katika msimu wa kilimo wa
mwaka 2010/2011 na mwaka 2013.
Nitume
aliiambia mahakama kuwa washtakiwa waligugushi lisiti za vocha za pembejeo
kwa kuwadangaya wananchi 294 wa kijiji cha Liugai kusaini vocha kama walipokea
vocha za pembejeo kwa manufaa binafsi huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria chini ya kifungu 333/335(d)(i) na kifungu 337 cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa kanuni namba 16 kama ilivyopitiwa mwaka 2012.
Aidha Nitume aliongeza kuwa watuhumiwa hao
wanakabiliwa na makosa mengine yakiwemo ya kula njama chini ya kifungu cha 32
cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na kutumia
nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mengine ni ubadhirifu, uchapuzi, kugushi
vocha 150 zikiwepo vocha 50 za mbolea aina ya DAP, UREA vocha 50 na vocha za
mbegu 50 na kuisababishia serikali
hasara ya shilingi milioni 3.3 huku wakujua kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria.
No comments:
Post a Comment