Na
Bazil Makungu Ludewa
MADIWANI
katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wameshindwa
kutunisha misuri kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo baada ya
kulazimisha na kudai bila mafanikio mambo yaliyo juu ya uwezo huku
wengi wao wakiwa mbumbumbu juu ya sheria na kanuni zinazoendesha
halmashauri.
Hayo
yalijitokeza katika balaza kuu la madiwani la robo ya pili ya mwaka
lililofanyika Aprili 12 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ambapo
pamoja na mambo mengine madiwani hao walimlalamikia mkurugenzi wao
Waziri kwa tabia ya kupuuzia maagizo mengi ikiwemo kutotekeleza agizo
lao la kumtaka atafute fedha mahali popote kwa ajili ya ziara ya
kujifunza katika maeneo yenye madini nchini kama vile Bulyankhulu na
kwingineko.
Aidha
hali ya hewa ilianza kuchafuka zaidi baada ya balaza hilo kumwagiza
tena mkurugenzi huyo kutafuta fedha mahali popote kwa ajili ya
kuwapeleka baadhi ya madiwani na wataalamu kwenda kukagua barabara ya
Amani hadi Ibumi waliyodai kutengenezwa na mkandarasi chini kiwango.
Ni
kutokana na agizo hilo ndipo madiwani walionesha udhaifu na uelewa
mdogo wa mambo ikiwemo usahaulifu unaotokana na ukosefu wa umakini na
kutokujali maslahi ya halmashauri yao hasa katika utoaji maamuzi
yasiyo ya msingi bila kujali uwezo na pato la halmashauri yao.
Hata
hivyo madiwani wachache wenye uelewa walionekana kukubali matokeo
huku wengine wakibaki bila kuonesha msimamo wao baada ya kugundulika
kuwa maagizo kama hayo yalikwisha kutolewa katika kamati ya uchumi,
mipango na fedha, kwa hiyo agizo la balaza lilikuwa la pili yaani
agizo juu ya agizo jambo lililomchanganya na kumshangaza mkurugenzi
na kushindwa atekeleza agizo gani kati ya hayo mawili.
Akijibu
na kutoa ufafanuzi wa maagizo ya madiwani hao mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Ludewa William Waziri alisema agizo kama
hilo lilikwishatolewa na kamati ya uchumi mipango na fedha kwa
kuagiza kuwa ni madiwani wawili tu wa kata ya Ibumi na kata ya
Mundindi ambako barabara hiyo inajengwa.
“”” waheshimiwa
madiwani nashindwa kuelewa nitekeleze agizo gani maana kamati ya
uchumi mipango na fedha iliagiza kitu kingine na balaza limeagiza
kitu tofauti hata hivyo wakienda madiwani na wataalam kukagua
hakutakuwa na ufanisi ni vema wakahusika madiwani wa kata
zinazoguswa na mradi huo ili kupunguza gharama.’’’’’
alisisitiza Waziri
Kufuatia
mvutano huo ndipo mwanasheria wa Halmashauri ya ya wilaya ya Ludewa
Nathani akaomba mwongozo wa mwenyekiti na kusoma kanuni namba 45
inayoelekeza uundwaji wa kamati ndogo na madaraka yake ambapo kanuni
hiyo inaeleza wazi kwamba kamati ukishatoa maelekezo balaza haliwezi
kutengua mpaka iamuriwe vinginevyo
Agizo
lingine lililoleta utata na kuwa ngumu kutekelezeka ni lile na
madiwani kumtaka mkurugenzi huyo kumwita kwa barua katibu mkuu wa
wizara ya nishati na madini kuja kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu
kushindwa kutekeleza agizo la rais la kufungua ofisi ya madini
wilayani Ludewa baada kumwita kamishna wa madini kanda ya nyanda za
juu kuhudhuria balaza bila mafanikio.
Maagizo
kuhusu matumizi ya fedha yanatolewa na madiwani hao yamekuwa
yakitolewa bila kuangalia uwezo wa halmashauri yao ingawa mkurugenzi
huyo amekuwa akikubali nakuahidi kuyafanyia kazi kila anachoagizwa.
Halmashauri
inategemea vyanzo vichache sana vya mapato ya ndani hata hivyo
inapata fedha kidogo sana kutoka serikali kuu na fedha za uendeshaji
halmashauri ni zaidi ya miezi miwili hazijaletwa jambo linalopelekea
hata vikao vya madiwani kushindwa kufanyika kwa wakati pamoja na
halmashauri kuidai bila mafanikioNFRA jumla ya shilingi m.400.
mwisho
No comments:
Post a Comment