POLISI
AUA RAIA KWA SMG ALITOROKA LINDO BENKI
.
Wananchi wagoma kuuzika mwili hadi kamati ya ulinzi na usalama ifike
.Mgogoro
mkubwa na visa vyatawala kati ya polisi na raia
.
Dc awaomba radhi wananchi na kuwataka wapunguze jazba sheria
itafanyakazi
Na
Bazil Makungu Ludewa
ASKARI
mwenye namba G 6352 Police constable Abduel wa kituo cha polisi
Ludewa katika mkoa wa Njombe, january 23 mwaka huu majira ya saa saba
za usiku alimpiga risasi kifuani na kufariki dunia hapohapo kijana
ajulikanaye kwa jina la Januari Mtitu 20 fundi magari mkazi wa mtaa
wa mdonga mjini Ludewa.
Akizungmza
katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Ludewa ambaye ndiye mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa Juma Madaha
alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari askari
anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ameshakamatwa na raia wengine
wawili kwa uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.
Madaha
aliwataka wananchi kupunguza jazba kufuatia tukio hilo na kwamba
wasiwazuru askari wenzake kwa sababu siyo wote waliohusika kutenda
kosa hili. Madaha alitoa kauli hiyo kufuatia mafundi kugoma
kutengeneza jeneza na kutaka kuandamana huku wakitaka jeshi la
polisi kutengeneza wenyewe ama kulipa fedha kwanza ndipo watengeneze.
’’’ tumechoka
kuteswa kunyanyaswa na polisi sababu wao wanaacha kukamata wahalifu
sasa wanawageukia wananchi wasio na hatia kwa kuwakamata na kuwatoza
fedha bila huruma na leo wameamua kumuua mwenzetu tunataka kujua
hatma ya askari huyo haraka.’’’’’ walisikika wakimweleza
mkuu wa wilaya.
Imani
d/o Mtitu mdogo wa marehemu yeye anasema kabla ya kakake kupigwa
risasi alisikia akiongea na mtu kwa njia ya simu huku wakijibizana
kwa ukali na baada ya muda walifika watu wakagonga mlango wa marehemu
na alipokataa kufungua walivunja mlango na muda mfupi ulisikika mlio
wa bunduki. ‘’’’ nilipotaka kutoka nje kumsaidia kakangu
mlango ulikuwa umefungwa kwa nje’’’ alisema kwa masikitiko
shuhuda huyo
‘’’’ nilipotaka
kutoka ili kumpa msaada kaka yangu niligundua kuwa mlango umefungwa
kwa nje na nilipofanikiwa kutoka nilikuta marehemu akiwa amelala
chini damu zinatoka lakini anashindwa kuongea.’’’’ alisema
Imani
Naye
mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa mrakibu mwandamizi wa polisi Gali ya
Moshi akizungumza na gazeti hili alisema chanzo cha tukio askari
Abduel Nyuki akiwa kazini kulinda benki ya NMB tawi la Ludewa
alipigiwa simu na mpangaji mwenzake kwamba katika chumba chake
kulikuwa kunafanyika wizi ndipo askari huyo aliacha lindo majira ya
saa saba usiku na kumfuata marehemu nyumbani kwake baada ya kuambiwa
na rafiki zake kuwa ndiye aliye husika.
‘’’’ pamoja
na askari Abduel wapo raia wawili Juma Mhagama na Rashidi Hamadi
ambao ndiyo waliomtaja marehemu kuwa mwizi na walimpeleka askari
nyumbani kwa marehemu na walikuwepo wakati tukio hilo likitendeka.
‘’’ alieleza Gari ya moshi
Habari
za kipolisi zinasema kuwa marehemu January Mtitu alikutwa na
vielelezo kadhaa mfukoni mwake ikiwa ni pamoja na Flashi na Remote ya
Tv vitu ambavyo vilitambuliwa na mshitakiwa aliyemuua marehemu askari
no G 6352 pc Abduel Nyuki kuwa ni mali yake.
Taarifa
za kipolisi zinaendelea kudai kuwa mbali na vielelezo hivyo kofia ya
mzazi wa marehemu (pama) ilikutwa nyumbani kwa askari huyo na
inadaiwa kuwa tangu mchana marehemu alikuwa ameivaa kwa hiyo kuna
uwezekano mkubwa wa marehemu kuiangusha wakati akitekeleza wizi huo.
Hata hivyo tv ya askari ilikutwa imefichwa kwenye pagale na nyumba
mbovu
Hata
hivyo wakati askari wakimtuhumu marehemu kuwa alikuwa mwizi wananchi
wamepinga vikali taarifa hiyo na kuongeza kuwa January Mtitu hakuwa
na tabia ya udokozi hata kidogo hivyo ameonewa na kuongeza kuwa
mauaji hayo yalipangwa na polisi kutokana na kuhofu kuwa marehemu
angetoa siri ya wizi wa gia box ya gari la polisi PT 0764 IR 00011
Landrover mbovu.
‘’’’ askari
wa kituo cha polisi Ludewa mjini walikuja kuchukua mafundi wawili
ambao ni Bruno fundi pikipiki na Yohana Mtitu ili kuwasaidia kufungua
gia box ya gari ya polisi na haikujulikana kama kifaa hicho kilikuwa
kinapelekwa wapi ingawa baadaye habari zisizothibitika zilisikika
kuwa kifaa hicho kilizua kesi ndani ya jeshi polisi mkoa.’’’’’
walisema wakazi wa Ludewa ambao hawakupenda majina yao yaandikwe
Hata
hivyo polisi walikiri kufunguliwa kwa kifaa hicho kwa njia ya
utaratibu wa kawaida wa kipolisi na siyo kwa njia ya wizi na kwamba
gia box hiyo imefungwa katika gari la polisi lililopo katika kituo
cha polisi Makambako na kwamba marehemu hakuwa mmoja kati ya mafundi
waliofika kufungua kifaa hicho kwa hiyo hakuna mahusiano yoyote ya
chuki kati ya polisi na marehemu.
Bruno
Paulo fundi magari anasema mwaka jana dereva wa polisi aitwaye Steven
alikuja gereji kwetu na kutuomba mimi na Yohane Mtitu twende
kumsaidia kufungua gia box na vifaa vingine katika Landrover PT 0764
na tulipomaliza tulilipwa shilingi 20,000 na vifaa hivyo viliwekwa
ktk gari ya polisi na kupelekwa Njombe ambako baada ya muda nilisikia
vikamatwa na dereva wa polisi kuwekwa mahabusu.
‘’’ Siku
hiyohiyo amri kutoka polisi mkoa njombe ilitolewa tu kamatwa na
askari hadi kituoni ambapo tulikaa mahabusu kuanzia muda wa saa tano
asubuhi hadi saa kumi na moja jiaoni ambapo tulitolewa kwa amri ya
mkuu wa wilaya ya Ludewa baada ya kuwataka askari waeleze sababu ya
kutuweka mahabusu wakati wao ndio waliruhusu kufunguliwa vifaa vya
gari. Alieleza Bruno
Marehemu
alizikwa katika makaburi ya Lugarawa mbele ya kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya baada ya mvutano mkali uliokuwepa kati ya wananchi
wa kijiji cha Lugarawa wazazi na jeshi la polisi ambao walikuwa
wakituhumiwa kumuua kwa makusudi marehemu January Mtitu.
Polisi
wilayani Ludewa wamekuwa wakipewa lawama kwa kutokuwa makini na
wawazi katika utendaji wao wa kazi kiasi cha kuzua lawama zisizo za
msingi matukio yaliyozua tafrani na kuleta sintofahamu ni pamoja na
kesi ya mbwa kumla hadi kumuua mtoto Ibrahimu chipungahelo ambaye
hadi sasa haijulikani hatma ya kesi hiyo.
mwisho


No comments:
Post a Comment