Thursday, October 25, 2012
CAF YATANGAZA MAKUNDI YA AFCON 2013
WALE WABABE wa Cameroun, Kisiwa kidogo cha Cape Verde, ambao wanacheza Fainali yao ya kwanza kabisa ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, wamepangwa Kundi moja na Wenyeji Afrika Kusini katika Droo iliyofanyika jana na wao ndio watafungua dimba Mashindano hayo kwa Mechi rasmi ya ufunguzi dhidi ya Afrika Kusini hapo Januari 19, 2013, ndani ya Soccer City, Soweto, Johannesburg.
Mabingwa watetezi Zambia wamepangwa Kundi moja na Timu ngumu Nigeria katika Kundi C pamoja na Ethiopia na Burkina Faso.
Vigogo wengine Ghana wamepangwa pamoja na Congo DR, Niger na Mali katika Kundi B.
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
MABINGWA AFRIKA:
2012: Zambia
2010: Egypt
2008: Egypt
2006: Egypt
2004: Tunisia
2002: Cameroon
2000: Cameroon
AFCON 2013 itachezwa Afrika Kusini kuanzia Januari 19 hadi Februari 10 kwenye Viwanja ambavyo vilitumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa Nchini humo.
Viwanja hivyo ni pamoja na FNB cha Mjini Johannesburg, Moses Mabhida huko Durban, Mbombela ya Nelspruit, Nelson Mandela Bay ya Port Elizabeth naRoyal Bafokeng ya Rustenburg.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment