Friday, October 26, 2012

KADA WA CHADEMA ARUSHA AJIUNGA NA CCM

Aliyekuwa mwenyekiti mtendaji mkoa wa Arusha kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema James Ndarvoi amekiama rasmi chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi(CCM)kwa madai kuwa chama hicho kimegubikwa na chembechembe za ukabila
Hatu hiyo ilikuja hivi karibuni katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendela katika kata ya daraja mbili Mkoani Arusha ambapo Ndarvoi alitangaza rasmi kujiunga na CCM
Alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kinaendeshwa kama taasisi ,huku akidai kuwa chama ni kwaajili ya wanachi na siyo ya mtu kukimiliki au taasisi
“chama cha chadema ni kama taasisi ya watu flani na kinachembechembe za ukabila ndani yake “alisema
Alidai kuwa chama cha CCM kimemtoa mbali huku akisisitiza kuendeleza amani na utulivu ndani ya chama hicho kwa kuwa yeye ni kijana na atashirikiana na wanachi katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi
“Wanachama waliopo chadema wahame haraka sana kwasababu wataendelea kutumika katika chama hicho kama daraja la kupitia tu, huku wakiwapendekeza watu wao kugombea nafasi za uongozi “alisema ndarvoi
Kwa upande wake katibu wa chadema Mkoa wa Arusha  Amani Golugwa alikana kumtambua ndarvoi huku akidai kuwa hajawai kuwa mwanachama wao
Golugwa alisema kuwa awali alikuwa amejiunga na CCJ na siyo chadema kama alivyodai kuwa alikuwa mwanachama wao
“Nasema hivi hajawahi kuwa mwanachama wetu na simtambui kama mwanachama wetu,kunakipindi flani alitaka kujiunga na chadema na siku ya kuchukuwa kadi hakuja kuchukuwa na baadae nilipata taarifa kuwa alijiunga na CCK kipindi hicho”alisema Golugwa

No comments:

Post a Comment