NDOTO na furaha za
wananchi na askari polisi wilayani Ludewa katika mkoa wa njombe kuhusu ujenzi
wa kituo kipya pamoja na nyumba za
watumishi zimetoweka kutokana na majengo hayo kutelekezwa zaidi ya miaka minne
bila kukamilika.
Aidha majengo hayo
badala ya kuishi askari sasa yamekuwa magofu na mapango ya kuishi panya na
wanyama wengine huku majengo hayo yakigeuzwa madanguro ya kufanyia ukahaba kwa
vijana na watu wazima wanaokwepa kutumia nyumba za kulala wageni kwa hofu ya
kuonekana na wake zao.
Wakizungumza na gazeti
hili kwa nyakati tofauti wananchi wanaoishi nyumba moja na askari hao, walisema
wamechoshwa na kuishi jirani na walinda usalama hao kutokana na tabia zao za
kuwalazimisha raia kufuata amri zao.
“” tunaomba serikali
imalizie ujenzi wa kituo cha polisi pamoja na nyumba za askari ili tuondokane
na kero hizi vinginevyo wasijekushangaa siku moja kutokea mapigano kati ya
askari wa uraiani na wananchi hususani wamiliki wa nyumba na vibanda vya
kupanga.”” Alisema mama Haule mkazi wa
kitongoji cha Ibani katika kata ya Ludewa mjini
Wakizungumza kwa
masharti ya kutoandikwa majina yao kwa kuwa wao si wasemaji wa jeshi hilo
askari polisi wilayani Ludewa waliilalamikia tabia ya jeshi hilo kutelekeza
jingo bila sababu ya msingi huku wao wakiendelea kuishi uraiani na kutumia
nyumba ya mtu binafsi isiyo na sifa kuwa ndiyo kituo cha polisi jambo ambalo ni
hatari kwao na washtakiwa.
“” sisi tunashangaa
serikali kujenga vipande vipande, ni wazi na kila mtu anaamini kwamba jengo
lolote la serikali linapoanza kujengwa bajeti yake huwa imekamilika kwa kuwa
mipango na bajeti vilikwishaainishwa na kupitishwa kwenye vikao halali sasa
inakuwaje ujenzi kusimama miaka minne?”” Aliuliza askari mmoja anayeishi nyumba
mbovu za kupanga uraiani kutokana na uhaba wa nyumba Ludewa
Fulgence Ngonyani ni
kamanda wa polisi mkoa wa njombe kwa upande wake akasema askari na wananchi
wawe watulivu kwa sababu serikali inakabiliwa na ufinyu wa bajeti na kwamba ana
imani majengo hayo yatakamilika pindi bajeti itakaporuhusu.
“” tatizo ni suala la
upatikanaji wa fedha bajeti inayotolewa haijatosheleza kuendelea kumaliza hapo
hata hivyo sijui gharama ya majengo hayo, ninachojua kuna miradi inakwenda kwa
awamu hakuna fedha iliyotengwa moja kwa moja.””
Akaongeza kamanda Ngonyani
CLODWIG MTWEVE ni
kamishina wa utawala na usimamizi wa raslimali za jeshi la polisi nchini
akasema bajeti ndogo na hali mbaya ya uchumi ndiyo vinavyofanya kuchelewa kwa
kumalizika kwa miradi iliyoanzishwa na serikali kwani kila mwaka fedha huidhinishwa
kwa ajili ya kumalizia viporo lakini wakati mwingine mambo ya kitaifa yanaingilia inabidi kusubiri tena.
“” gharama ya mradi
inaweza kufahamika nap engine kupangwa kufanyika kwa muda Fulani na ile bajeti
hugawanywa kulingana na kila mwaka wa fedha sasa inapotokea majukumu ya kitaifa
inabidi miradi mingine isimame lakini naamini katika mwaka wa fedha ujao
serikali itaweza kumalizia mradi huo.”” Akasisitiza kamishna mtweve
Kwa mujibu wa
mkurugenzi wa kampuni ya MNM engeneering Ltd Joseph Msangi mradi huo mpaka
kukamilika utagharimu zaidi ya shilingi 800 milioni.
mwisho
No comments:
Post a Comment