USHURU
WA MABANGO WAJA LUDEWA, MARUFUKU KULIMA MAHINDI MJINI.
Na Bazil Makungu Ludewa
MKURUGENZI
mtendaji katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Fidelis Lumato
amewataka wafanyabiashara kujiandaa kutoa ushuru wa kulipia mabango yaliyopo
kila kona ya mji kama njia ya kuongeza mapato ya ndani kwa halmashauri hiyo.
Kimato
aliyasema hayo ofisini kwake jana ambapo gazeti hili lilitaka kujua mikakati
yake hasa katika kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo kutokana na
kutegemea ruzuku kwa asilimia kubwa huku wananchi wakikosa baadhi ya huduma
ambazo ziko chini ya uwezo wa halmashauri.
Pamoja
na hayo Lumato alisema kunamajukumu mbalimbali ambayo anapaswa kuyatekeleza
ambayo ni kusimamia utekelezaji wa miradi
iliyopangwa na selikali,ufuatiliaji wa wawekezaji wa makaa ya mawe
mchuchuma,kuboresha mazingira ya kazi na kuhakikisha bajeti iliyotengwa na
selikali kwaajiri ya watumishi wa umma inatumika ipasavyo
wananchi Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wameaswa kuacha kubweteka na kushinda kutwa
wakinywa pombe badala yake wafanyekazi
kwa bidii ili kuondokana na umaskini wa kipato unaowakabili.
Akizungumza
na kipindi hiki ofisini kwake jana Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Ludewa Fidelis Lumato amewataka wananchi kutambua
kutumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuandaa mashamba mbegu na
mbolea ya kupandia ili kuendana na msimu wenyewe.
Aidha
Lumatto akawahimiza wananchi kujiandaa kunufaika na fursa za kujikwamua na
umaskini zinazotarajia kupatikana kutokana wawekezaji katika migodi ya makaa ya
mawe ya mchuchuma na chuma cha Liganga inayotegemea kupokea wageni wengi wa
ndani na nje ya nchi.
Fursa
zilibainisha na wataalamu ni pamoja na sekta ya kilimo, utalii,ufugaji nyuki,uvuvi
na misitu,
Hata
hivyo Lumatto alikiri kwamba wananchi wa Ludewa hususani wanaoishi katika
maeneo ya uwekezaji hawana elimu ya kutosha na wala hawajitambui kuhusu fursa
zinazotokana na migodi hiyo kwa sababu
bado hawajaandaliwa vya kutosha.
Kuhusu
halmashauri yake kuwa na vyanzo vichache vya mapato mkurugenzi alisema amekuta
halmashauri ya wilaya ya Ludewa imechoka hivyo anategemea kubuni vyanzo vipya
vya mapato ikiwemo kutoza kodi na ushuru wa mabango ambayo kila kukicha yamekuwa
yanazaliwa na kuongezeka na kwamba atasimamia kwa karibu maafisa watendaji kata
na vijiji kuliko ilivyokuwa awali.
Lumato alisema kuwa licha ya kuwa na
vyanzo vidogo vya mapato wilayani humo
kuna wawekezaji ambao wameingili kati kulipa mapato hayo kutokana na uchimbaji wa makaa ya mawe
mchuchuma hata hivyo inawapa shida
kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara.
Pia bw. Lumato alisema kutokana na
wawekezaji walioingia walayani hapo bado kunachangamoto ya uhitaji mkubwa wa
mahoteli ya vyakula na uzalishaji wa vyakula kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya
wawekezaji hao.
,,Wananchi hawajandaliwa na kujipanga
vizuri katika uchimbaji wa madini ila
tunatarajia kuleta wafanyakazi wanje ya nchi
1,000 na wa ndani ya nchi 3,000
ili kufanikisha uchimbaji wa madini
hayo bw. Fidelis alisema’’.
Pamoja na hayo bw.Lumato alisema
kunamajukumu mbalimbali ambayo anapaswa kuyatekeleza ambayo ni kusimamia
utekelezaji wa miradi iliyopangwa na
selikali,ufuatiliaji wa wawekezaji wa makaa ya mawe mchuchuma,kuboresha
mazingira ya kazi na kuhakikisha bajeti iliyotengwa na selikali kwaajiri ya
watumishi wa umma inatumika ipasavyo.
Aidha kuhusiana na wafanyakazi
wa afya bw.Lumato alisema kuwa kunaupungufu wa
watumishi wa afya na zahanati katika
wilaya nzima ya ludewa ambapo kuna
watumishi yapata 378 na tatizo hilo lipo nje ya uwezo wake kwani hana mamlaka
ya kumwajiri mfanyakazi isipokuwa
kusimamia.
Alisema sabababu nyingine kubwa ya
kukosekana kwa wafanyakazi wilayani hapo ni kutokana na kutoridhia hali ya
maisha ya ludewa kwani utakuta mfanyakazi
mwajiriwa amepangiwa kituo lakini akiona hali ya maisha ya pale ni ngumu
anathubutu kwenda sehemu ambayo hajapangiwa afanye kazi.
Bw. Lumato Alisema kutokana na sheria
ya selikali kama mfanyakazi mwajiriwa anajipangia kituo wao hawana mamlaka yoyote ya kuweza kumsaidia
isipokuwa arudi katika kituo cha afya kilekile alichopangiwa kwani akienda
kinyume na sheria anaweza kukosa kazi kabisa na kutotambulika tena kama mtumishi wa selikali.
Ili kupunguza tatizo la kutokuwa na
wafanyakazi wa vituo vikubwa vya afya na
zahanati wilayani Ludewa Bw.
Fidelis Lumato anaiomba selikali
kuliangalia tatizo hili kwa kuwapeleka
wafanyakazi kwa kuwa tatizo hilo lipo
juu ya uwezo wake.
MWISHO
KAMATI YA TUZO YA RAIS YATEMBELEA LIGANGA MCHUCHUMA
Na Bazil Makungu
WANANCHI wa wilaya Ludewa katika mkoa wa Njombe wameieleza
kamati ya tuzo ya rais wasiwasi na kusikitishwa kwao juu ya mikataba ya siri
inayowekwa kati ya Serikali na wawekezaji huku wao wakibaki watazamaji kwa
kutojulishwa kila hatua inayoendelea kwenye migodi ya makaa ya mawe ya
Mchuchuma na chuma cha Liganga.
Hayo yamesemwa jana na wananchi wa kata ya Mundindi mbele ya
mwenyekiti wa kamati ya Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na uwezeshaji Dr.Rumisha Kimambo katika ziara ya tume hiyo
wilayani Ludewa kwenye migodi ya makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma kilichoko
liganga.
Tume hiyo yenye wajumbe saba wakiwemo majaji wastaafu inafanya
ziara nchi nzima ikikukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wanaoishi
katika maeneo ya migodi,wawekezaji na Serikali kwa upande mwingine katika
katika kutekeleza mpango wa mafiga matatu.
Wananchi wa Ludewa pamoja na mambo mengine walitaka kujua ni
lini machimbo yataanza lakini wakataka kujua nini kilichomo kwenye mikataba na
vipi wao watanufaika kupitia wawekezaji wanaotarajia kuchimba migodi ya Makaa
yamawe ya mchuchuma na chuma cha Liganga kama wataweza kutambua fulsa zilizopo
na kuzifanyia kazi.
Akijibu maswali Dr.Kimambo alisema kamati hiyo ya rais ina
kazi ya kutembelea katika migodi mbalimbali nchini ili kuona kama wananchi wa
maeneo ya migodi wananufaika na miradi hiyo ikiwa ni mpango wa Serikali kuona
uwekezaji nchini unaleta faida kwa watanzania.
Alisema dhana ya mafiga matatu ni pana ambapo figa la kwanza
ni mwananchi kuzitambua fulsa zilizopo migodini na kuzitumia,figa la pili ni
mwekezaji kuhakikisha jamii inanufaika na uwekezaji wake ikiwa ni kujenga
miondombinu ya maji,shule,hospitari na mambo mengine na figa la tatu ni
Serikali kusimamia sera ya nchi katika uwekezaji.
“”Serikali ingependa kuona wananshi wake wananufaika na
uwekezaji ulioko nchini na si migogoro inayoendelea kati ya wananchi na
wawekezaji hivyo ikaona ni vyema kuunda chombo kinachofuatilia mambo
yanayopaswa kufanywa na pande zote mbili yenye tija kwa nchi””,alisema
Dr.Kimambo.
Dr.Kimambo alisema kamati hiyo ilianzia kuitembelea migodi ya
kanda ya ziwa na itatembelea nchi nzima ili kuona kwa miaka mitatu wawekezaji
wamefanya kitu gani kwa wananchi hasa katika huduma za jamii na kuondoa
migogoro inayotokea kati ya wananchi na wawekezaji.
Naye Catherine Lyombe mratibu wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na
Uwezeshaji(CSRE) akawatoa wasiwasi wananchi na kusema Rais Kikwete alizindua tume hiyo ili kuweka uwazi
katika miradi ya wawekezaji kwa kuwa wananchi wanapaswa kutambua faida za miradi
hiyo kwa jamii.
Hata hivyo Catherine aakawahakikishia kwamba kupitia tuzo hiyo basi kila mmoja atatimiza
wajibu wake ikiwa ni kuzingatia mikataba aliyoingia na Serikali kama inavyotaka
sera ya nchi kwa wawekezaji waliokwisha anza kazi katika migodi ya kwa zaidi ya
miaka mitatu.
Wananchi wa Ludewa hawawezi kunufaika sasa kwa sababu wawekezaji
bado katika utafiti lakini baada ya kumaliza tafiti zao na kuanza kazi za
uchimbaji ni lazima wazingatie mikataba waliosaini ili kuinufaisha jamii
inayoizunguka migodi ya chuma Liganga na makaa yam awe yaliyoko Mchuchuma.
Ni vema wananchi wa wilaya ya Ludewa waandaliwe ili waweze
kuzitambua fulsa walizonazo na wazifanyie kazi kwani haitapendeza kama hata
mayai, matunda, nyanya, maziwa na nyama
vitaagizwa kutoka katika maeneo mengine wakati wazawa wanao uwezo wa kuzalisha
bidhaa hizo na kuuza migodini.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na kuwaandaa wananchi mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha
alisema kupitia mradi wa PACA unaoendeshwa na shirika la maendeleo la
Taifa(NDC) wananchi wameanza kuandaliwa ili kuzitambua fulsa zinazowazunguka.
Bw.Madaha alisema mradi huo umeshapita vijijini na unaendelea
kuielimisha jamii jinsi ya kujitambua na kuandaa mipango ya kilimo na ufugaji
utakaowanufaisha wananchi kuuza bidhaa
zao migodini.
Alisema Kupitia MKURAIBITA wilaya Ludewa imeweza kutoa hati za kimila za ardhi
kwa wananchi 95 katika kata ya Mundindi kijiji cha Amani lakini mpango huo wa
kurasimisha ardhi wananchi unaendelea katika vijiji vingine.
Bw.Madaha alisema bado wataalamu wanaendelea kuwashauri
wananchi kutouza maeneo yao ovyo kwa wawekezaji kwani maeneo hayo yataweza
kutumika katika kuzalisha mazao na kuwauzia wawekezaji katika migodi.
Kamati hiyo imeondoka wilayani Ludewa ikielekea mkoa wa Mbeya
katika migodi mingine ili kuielimisha jamii na wawekezaji kutimiza malengo ya
tuzo ya Raisi katika Huduma za jamii na uwezeshaji.
MWISHO.
UHOLANZI YAKABIDHI MABWENI YA WASICHANA NA KUONGEZA
74 MILION
Na Bazil Makungu
UMOJA wa wanafunzi wa Uholanzi chini ya Shirika
lisilo la kiserikali la Shipo linalojishughurisha na kutoa huduma kwa jamii mkoani
Njombe limekabidhi mabweni mawili ya
wasichana yenye thamani shilingi 60 milioni kwa ajili ya Shule
ya Sekondari ya Mundindi wilayani Ludewa.
Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kike zaidi ya sabini yamejengwa
kwa ushirikiano kati ya mfadhiri huyo na wananchi wa kata ya Mundindi, umoja wa
wanafunzi wa uholanzi umekuja baada ya kukithiri kwa mimba na utoro kwa
wanafunzi wa shule ya sekondari ya mundindi kunakotokana na wachimbaji madini.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi afisa ufundi wa shirika la SHIPO Vincent Mgina ambaye ni Diwani wa kata ya Mundindi, alisema ujenzi
wa shule hiyo ulianza rasmi mwaka 2011 ambapo wanafunzi wa Uholanzi kupitia shirika
la SHIPO walianza kuchanga fedha na kuifadhiri shule hiyo na kujenga mahusiano
na wanafunzi wa mundindi.
Mgina alisema
kutokana na uhusiano mzuri ulijengwa kati ya wanafunzi wa Uhoranzi na wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Mundindi ndio uliowezesha shule hiyo kujengwa haraka
na kwa majengo mazuri tofauti na shule nyingine wilayani Ludewa.
Alisema wanafunzi wa Uholanzi kupitia shirika la shipo
walitoa vifaa vya vyote vya viwandani pamoja
na mbao wakati wananchi wa kata ya mundindi walijitolea nguvu zao ikiwemo
ufyatuaji wa tofali,uopoaji mchanga na ujenzi hali ambayo iliwatia moyo wafadhili
ambao walivutiwa na mwamko wa wananchi na sasa wamepanga kuendelea kuifadhiri
shule hiyo.
“shirika
letu limeona ushiriki wa wananchi wa Mundindi katika maendeleo yao kutokana na
wanavyojitoa kufanya kazi za ujenzi wa shule hii hivyo wafadhiri wanataka kuona
shule hii inaendelea kuwa bora zaidi ya shule nyingine katika wilaya ya Ludewa”,alisema
diwani Mgina.
Mgina alisema licha ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na
mabweni hayo shirika lake limetengeneza vitanda 35 vyenye uwezo wa kulaza
wanafunzi 70 lakini limeahidi kujenga mabweni manne na ukumbi wa kujisomea
utakaokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 274 .
Hata hivyo
ujenzi wa nyumba ya matroni na mabweni ya wanafunzi wa kike unaendelea ili
kupunguza uwezekano wa wanafunzi wa kike kupata ujauzito ambao utawakatishia
masomo yao.
Mathei Kongo ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
na ndiye aliyekuwa mgeni kwa upande wake aliwasisitiza wanafunzi, wananchi na wadau wa
maendeleo katika kata ya Mundindi kuitunza shule hiyo na vifaa vilivyomo kwa
kuzingatia shule hiyo imejengwa kisasa zaidi.
Mh.Kongo aliliomba shirika hilo kutengeneza uzio wa
kuizunguka shule hiyo kutokana kuwa
karibu na maeneo ya machimbo ya chuma cha liganga na mashimbo ya dhahabu kjiji
cha Amani ambako shule hiyo imejengwa.
Alisema uhusiano
mzuri walioujenga wanafunzi wa shule ya sekondari Mundindi na wanafunzi wa
Uhoranzi kupitia shirika la SHIPO unafaa kudumishwa ili kuleta changamoto ya
maendeleo katika kata nyingine zisizo na wafadhiri ambapo wataweza kuiga
utendaji kazi wa wananchi wa Mundindi.
Kongo akaishukuru
Uholanzi kupitia shirika la SHIPO kwa kutoa hundi ya shilingi za kitanzania 70
milioni katika hafla hiyo ili kuendeleza ujenzi wa nyumba ya matroni na mabweni
ya wasichana yanayoendelea katika ujenzi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment