Wednesday, December 26, 2012



HOSPITARI YA LUGARAWA YAKUMBWA NA UHABA WA WAGANGA. WALIOOPO WAFANYAKAZI MASAA 24.

                Na Bazil Makungu 

WATUMISHI katika hospitali ya  misioni ya Lugarawa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wanalazimika kufanyakazi bila kupumzika kutokana na uhaba na upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa kada mbalimbali hususani watabibu na wataalam wengine.

Akizungimza na gazeti hili jana mganga mkuu wa hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la njombe Dr Daudi Mwakalago alisema hospitsli yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo waganga ambapo hadi sasa anao waganga wasaidizi(Asissitant medical officers) wawili na mganga msaidizi (medical assistant ) mmoja tu.

‘’’’kutokana na uhaba huo waganga tunalazimika kufanyakazi masaa ishirini na nne bila kupumzika lakini kwa upande wa wauguzi hali siyo mbaya sana ukilinganisha na maafisa uuguzi hivyo tunaomba kuongezewa wathumishi ili kuongeza tija.’’’ Alisema Mwakalago

Aidha mwakalago akaongeza kuwa mbali na uhaba wa wauguzi katika hospitali hiyo bado wanakabiliwa na changamoto nyingine ya ugumu wa uendeshaji hospitali  kwa sababu wananchi wengi wa eneo hilo wanakabiliwa na umaskini wa kipato hali inayowafanya washindwe kumudu gharama za matibabu na kupelekea wengine kutoroka bila kulipia huduma za  matibabu na kusababisha hasara.

Kwa kawaida  Hospitari yetu hupokea wagonjwa mbalimbali wanaokuja kupata huduma hata kama hawana fedha  lakini kwa makubaliano ya kulipa baadaye lakini hukosa uaminifu na kuamua kutoroka bila kulipa ‘’’’’watu wetu kipato chao ni duni kwa hiyo siyo  wote wanaolipa madeni wengi wanatoroka kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu.’’’alilalamika Mwakalago
Alizitaja gharama za matibabu kuwa mama mjamzito anayejifungua kwa upasuaji (operation) ni shilingi elfu thelathini na tano(35,000)akina mama wanaojifungua kawaida shilingi elfu kumi na tano (15,000), upasuaji kwa wagonjwa wa kawaida ni shilingi sabini elfu(70,000) zikiwemo gharama za malazi.

Kwa wagonjwa ambao ni wanachama wa bima ya afya wanalazimika kulipa shilingi laki moja na sitini elfu(160,000) kiwanga ambacho ni kidogo sana ukilinganisha na sehemu zingine za mjini. 

Dkt.Mwakalago alisema Hospitali hiyo iliyoanzishwa na wamisionari bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa wafanyakazi na kukosa fedha za kujiendesha kutokana na kukosa ufadhiri kwa muda mrefu sasa.

Kuhusu fedha  toka Serikalini alisema Hospitari hiyo haijapata  fedha hizo zaidi ya miezi saba sasa hivyo uendeshaji wa kazi katika vitengo vya mama na mtoto umekuwa mgumu ambapo inawalazimu kuwatoza kiasi cha shilingi elfu tano kwa watoto katika kuchangia huduma za Afya.

Licha ya changamoto zinazo ikabili Hospitali hiyo Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe ametoa msaada wa mashuka 162 ambayo yatatumiwa katika vitanda vya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.

Akitoa msaada huo Bw.Filikunjombe alisema ameguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo hivyo ameona vi vema kuona uwezekano wa kupunguza changamoto hizo na akaahidi ataendelea kufanya linalowezekana ili kuendeleza historia ya Hospitali ya Lugarawa.

Bw.Filikunjombe alijumuika na wagonjwa katika chakula cha mchana ili kuwafariji katika sikukuu ya X mas kwani aliweza kuona kazi wanazofanya wafanyakazi wa hospitari hiyo bila ya mapumziko kutokana na uchache wao.

Akishukuru kwa msaada wa mashuka na kandambili pea 100 alizozitoa Bw.Filikunjombe Dkt.Mwakalago alisema ni upendo wa kipekee aliouonesha Bw.Filikunjombe wa kutoa msaada huo na kula chakula na wagonjwa hivyo jamii inapaswa kuiga tabia hiyo.
Mwisho.



No comments:

Post a Comment