IMEKUWA desturi kwa
mbunge wa Ludewa Mkoani Njombe Deo Filikunjombe kula chakula na wagonjwa katika
Hospitali mbalimbali jimboni mwake wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka, lakini
Xmass ya mwaka huu aliwashangaza wagonjwa alipoanza kulia wodini.
Filikunjombe
alishindwa kujizuia pale alipoingia wodi ya watoto na kukutana na mtoto Diana
Haule (12) anayeteseka na vidonda vilivyoenea karibu mwili mzima vikitokana na
kuungua moto kunakosababishwa na ugonjwa wa kifafa.
Aidha hali ya simanzi
ilianza kujitokeza pale motto Diana alipoamua bila hofu kuonesha umahili,
kipaji na uwezo wake pale alioomba aimbe
wimbo maalumu kwa ajili ya mbunge ambao ulieleza mateso anayopata na kumwomba
mbunge ampe fedha ya matumizi.
Diana alimwambia
Filikunjombe kuwa awali aliangukia kwenye moto na kuungua viaya jambo
lililopelekea kukatwa gumba cha mkono wa kushoto, ambapo pia madaktari waliamua
kukata nyama kutoka kiunoni na kushona katika sehemu nyingine iliyoungua katika
mkono huo.
Akionekana mcheshi
asiye na uoga motto Diana aliwaliza wengi wakiwemo waandishi wa habari
walioongozana na msafara wa mbunge pale aliposema kuwa anapenda sana kusoma ili
awe kama watoto wengine lakini analazimika kuishi wodini kutokana na
kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu sasa.
DAUDI MWAKALAGO
mganga mkuu wa hospitali ya Lugarawa akitoa taarifa kwa mbunge alisema mtoto
Diana alilazwa hospitalini hapo tangu septemba mosi mwaka huu akiwa na jeraha
kubwa lililotokana na kuungua na moto katika mkono wake wa kulia.
Dr Mwakalago
aliongeza kuwa pamoja na ugonjwa unaomsumbua na maumivu makali aliyo nayo Diana
yeye na wafanyakazi wenzake wanapata faraja kubwa kutokana na motto huyo
kujieleza mwenyewe huku akiwatia moyo kwa kuonesha furaha na uchangamfu pale
anapopata matibabu.
‘’’’ kuna wakati hali
ya motto Diana ilibadilika nay eye mwenyewe akaomba kubatizwa haraka na ndipo
alibatizwa jina la Diana na kuachana na jina awali alilokuwa akitumia la Philipina
ambapo baada ya kubatizwa akaanza kuendelea vizuri.’’’’ Alieleza Dr Mwakalago
EMELENSIANA MTULO ni
mama mzazi wa Diana, akitoa historia ya mtoto alisema mwanaye alianza kuugua
kifafa mwaka 2003 na kuungua vibaya katika mkono wa kushoto ambapo alilazwa kwa
muda miezi saba akapona lakini mwaka 2011 akaanza kuugua kifafa tena na septemba
mosi mwaka huu aliungua tena na kulazwa.
‘’’’ mimi naomba
motto wangu apimwe ubongo kuona kama
umechanganyikiwa kwa sababu safari hii ameungua vibaya mkono wa kulia na kupelekea
madaktari kulazimika kuondoa mfupa mmoja ulioharibika.’’’’
DEO FILIKUNJOMBE kwa
upande wake akaahidi kuwasiliana na madaktari wanaomhudumia mtoto Diana ili apate
taarifa kamili na kisha ataaangalia namna nzuri ya kumsaidia na kuchangia kadri
mungu atakavyo mjaalia.
No comments:
Post a Comment