mvuvi wa samaki akiwa anatoka kuwavua samaki aina ya vitui wanaopatika katika ziwa nyasa
watoto wa kijiji cha mkongobaki wakifuatilia mkutano wa mbunge wa jimbo la Ludewa
katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Stanley Gowele akitoa utambulisho kwa wananchi kuhusiana na viongozi walioambatana na msafara wa Filikunjombe
Filikunjombe akimpongeza diwani wa kata ya Mkongobaki kwa kazi anazofanya mbele ya wananchi wa kata hiyo
kijana wa kabila la wakisi lililoko mwambao wa ziwa nyasa wilayani Ludewa akivua samaki kwa kutumia ndoano.
Filikunjombe akikagua nyumba ya mganga iliyojengwa chini ya kiwango katika kijiji cha Nkanda kata ya Lumbila wilayani Ludewa
Filikunjombe akijadiliana jambo na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe katika ziara yake kushoto ni Baba mzani wa mbunge huyo
Filikunjombe akiteta jambo na mpigapicha wa gazeti la Mwananchi Bw.Said
Filikunjombe akiwa ndani ya boti tayari kwa safari ya kutembelea kata nne za mwambao wa ziwa nyasa
jengo la shule ya msingi Chanjale kata ya Lumbila wilayani Ludewa likiwa katika hali mbaya kiasi ambacho ni hatari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Filikunjombe akiselebuka ngoma ya Ngwaya maalufu kwa kabila la Wapangwa lililoko wilaya ya Ludewa.
Filikunjombe akiwa na viongozi wa kata ya Madope katika moja ya ziara zake
safari ni safari hapa Filikunjombe akiwa ndani ya mtumbwi na katibu mwenezi wa wialaya ya Ludewa Bw.Mtega wakielekea kupanda boti tayari kwasafari ya kata nyingine.
Filikunjombe akiwaangalia wananchi waliokuja kumpokea katika kijiji cha chanjale hawako pichani.
wananchi wakifanya maandamano ya kumpokea mbunge wao
Filikunjombe akishuka katika boti tayari kwa mkutano
kijana mdogo akisafiri kwa mtumbwi katika ziwa nyasa,ni usafiri unaotumika katika maeneo hayo.
wanafunzi wa shule ya msingi Chanjale wakiwa darasani,jengo ambalo limepasuka na nihatari kwa maisha yao.
vyoo vya shule ya msingi Chanjale wilayani Ludewa vikiwa katika hali mbaya
No comments:
Post a Comment