Thursday, January 10, 2013

WACHINA WAKARABATI SHULE YA MSINGI ILIJENGWA MWAKA 1974




                 Na  Bazil Makungu

KAMPUNI ya Tanzania China Internation Minerals Resouces Limited (TCIM) inayochimba madini ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga Ludewa imeanza ukarabati wa shule ya msingi katika kijiji cha Mkomang’ombe wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe baada ya wananchi kushindwa wa kijiji hicho kushindwa gharama.

Shule ya msingi Mkomang’ombe iliezuliwa paa lake na vyumba vitatu kuharibiwa vibaya kutokana na upepo mkali kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Ludewa na kusababisha uharibifu mkubwa ambao kwa mujibu wa uongozi wa kijiji wananchi walishindwa kumudu gharama za ukarabati.

Akikabidhi mabati na misumari na vifaa vya ujenzi kwa wananchi wa kijiji cha mkomang’ombe meneja mkuu wa uzalishaji wa makaa ya mawe na umeme Achen qi Hong alisema kuwa kampuni yake imeaua kutoa vifaa vya kiwandani kama mchango wa ukarabati wa shule hiyo baada ya kuona watoto wanakosa mahali pa kusomea.

’’’’ Tanzania na China mbali ya ubia uliopo katika miaradi ya Liganga na mchuchuma tuna udugu wa muda mrefu kwa hiyo watoto wa kijiji cha cha mkomang’ombe wanapokosa masomo tunaathirika sote kwa sababu ni watoto wetu sote.’’’’ Alisema Achen Hong

ZHAO DAO QUAN mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Tanzania China International Menerals Limited na HUANG DA XIONG ambaye ni afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo wakaliambia gazeti hili kuwa walipokea barua kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mkomang’ombe wakiomba mchango wa vifaa vya madukani sisi hatukua na pingamizi kwani ni sehemu ya mahusiano yetu na wananchi.

‘’’’’ huo ni mwanzo tu si kama wawekezaji tutaendelea kushirikiana na wananchi na jamii kwa ujumla katika masuala yote ya maendeleo yakiwemo elimu, Afya na maji kwa kuwa ni mahitaji muhimu ya binadamu.’’’ Alisema Zhao mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mkomang’ombe John Haule akitoa taarifa kwa wadhiri hao alisema shule hiyo imejengwa mwaka 1975 kwa ramani za wakati huo lakini shule hiyo imekuwa ikiezuliwa na upepo kila mwaka jambo ambalo kila likiezuliwa inakuwa mzigo wa wazazi ambao hushindwa kumudu gharama kutokana na kukabiliwa na umaskini wa kipato.

Haule akaongeza kuwa kijiji kilipitisha mchango wa shilingi mia tano (500) kwa kila mwananchi lakini fedha iliyochangwa haikutosha kununua hata kilo moja ya misumali ndipo tukaomba msaada kwa wenzetu wachina ambao hawakusita kutoa mchango huo.

‘’’’’ Taarifa ya kuezuliwa kwa shule hiyo kila mwaka tulishapeleka kwa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa lakini bado haijapatiwa ufumbuzi kwa hiyo tunaendelea kusuasua na ukarabati kila linapotokea tatizo kwa sababu uwezo wa kuivunja na kujenga upya hatuna.’’’’alisema Haule

Haule akaongeza kuwa wanalazimika kuweka zamu ya kuingia madarasani kwa wanafunzi hasa kwa darasa la sita, darasa la tano, na darasa la tatu na pili kutokana na uhaba wa madarasa kufuatia kuezuliwa kwa madarasa hayo.

Akitoa shukrani kwa kampuni hiyo Diwani wa kata ya Mkomang’ombe Ananias Haule Mamba alisema wananchi wa kata yake wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa katika sekta ya elimu afya na maji na kuongeza kuwa wawekezaji wameanza vyema hivyo ana imani watasaidia hata katika shughili zingine za maendeleo pale watakapotakiwa kufanya hivyo.

Kampuni ya Tanzania International Minerals Limited inaendeshwa kwa ubia kati ya Tanzania na China katika migodi ya uchimabaji makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha pua cha Liganga.
                                mwisho

No comments:

Post a Comment