MBUNGE wa Ludewa katika mkoa wa Njombe amewakemea vikali watendaji wasio
waaminifu wilayani Ludewa katika kutekeleza miradi ya ujenzi inayofadhiriwa na
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na ujenzi ulio chini ya
Viwango.
Hali
ilitokea wakati wa ziara yake katika kata za Mwambao wa Ziwa nyasa ambapo
aliweza kuona fedha zinazotolewa na Serikali ili kufanikisha mambo mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu na zahanati zikiwa zimetumiwa vibaya na
wasimamizi wa fedha hizo maeneo ya miradi.
Katika ziara
hiyo Filikunjombe aliweza kujionea ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nkanda na
nyumba ya mwalimu katika kijiji hicho kata ya Lumbila kujengwa chini ya kiwango
ambapo uchanganyaji wa saruji na mchanga haukukidhi viwango hivyo aliweza
kutomasa kwa kidole na kujionea ikipukutika kanakwamba ilijengwa bila ya
saruji.
Aliliona jengo
la nyumba ya kuishi mwalimu katika shule ya msingi Nkanda likiwa ninazaidi ya
mwaka mmoja bila kumalizika ndipo alipomtaka mkandalasi wa jingo hilo na
kuelezwa mkandalasi wa jingo hilo alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“Hatuwezi
kuuchekea ufisadi wa waziwazi kama huu,haiwezekani Serikali ikatoa fedha kwa
manufaa ya watanzania lakini watu
wachache wakanufaika na fedha hizo kwa kujenga majengo yasiyo na viwango wala
ramani inayokubalika na Srikali”,aliseema filikunjombe.
Aidha
alisikitishwa kuona nyumba ya mganga inayojengwa pamoja na zahanati ya kijiji
cha Nkanda kata ya Lumbila uchanganyaji wa saruji na mchanga hauna uwiano hivyo
kupelekea kuta zake kutokuwa imara wakati viongozi wa kijiji na kata wapo eneo
hilo na wanaona kinachoendelea bila kuchukua hatua za kisheria.
Filikunjombe
alisema kama kila mtanzania atakuwa mlinzi wa raslimali za nchi Tanzania
itasonga mbele kwani hali ya uchakachuaji wa fedha za miradi ya Serikali
haitakupo tena hivyo sera ya na
utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) itatekelezwa kama
ilivyokusudiwa.
Hata hivyo
mwalimu mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Andrea Nkwera alishikwa na kigugumizi katika
kulitolea ufafanuzi kuwa alijihusisha na ukandarasi wa kujenga nyumba ya
mwalimu akiwa hana taaluma ya ukandarasi na pasipo na ramani inayokubalika na
Serikali.
Mwalimu.Nkwera
alishindwa alishindwa kutolea maelezo baada ya kutakiwa kuonesha ramani ya
jengo hilo na BOQ ambavyo hakuweza
kuvitoa kutokana na ujenzi wa jengo hilo kutokuwa na vitu hivyo kama majengo
mengine ya Serikali yanavyo jengwa.
Aidha
Filikunjombe aliuagiza uongozi wa kata kufuatilia matumizi ya fedha hizo na
kumchukulia hatua za kisheria mwalimu huyo pamoja na kamati yake ya ujenzi kwa
kutofuata sheria za kiserikali katika ujenzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment