Na Bazil Makungu
WENYEVITI wa Serikali
za vijiji katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wameitaka serikali kuwalipa
posho au mishahara kwa kuwa wanafanyakazi ngumu na katika mazingira ya hatari na
yenye kila aina ya ushawishi.
Wakizungumza na
gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema kuwa wamekuwa wakifanyakazi ngumu
zenye lawama na hatari na wakati mwingine majira ya usiku kwa sababu tu ya kulinda
usalama kwa wananchi.
Mzee Mwafute (56) ni
mwenyekiti wa kijiji cha Lusitu katika kata ya Madope Tarafa ya Mlangali kwa
niaba ya wenyeviti wilayani alisema wenyeviti wa vijiji pamoja na wenyeviti wa
vitongoji ndiyo wenye watu hata adha na usumbufu wanaopata hauna faida hata
kidogo kwao na familia zao.
Kwa upande wake
mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akaenda mbaili zaidi na kusema wanaotakiwa
kulipwa posho siyo wenyeviti wa vijiji na vitongoji tu bali hata wazee ambao
wamelitumikia taifa hili lakini hawakuwahi kuajiriwa wanatakiwa kutambuliwa kwa
sababu wametoa mchango mkubwa katika Taifa kwa namna moja au nyingine.
‘’’’ wenyeviti wa serikali
za vijiji ni kweli kazi wanazofanya ni ngumu kwa hiyo kinachotakiwa ni serikali
kutambua uwepo wao na kuonesha ukarimu kwa kuwapa posho kama siyo mshahara ili
kutambua na kuthamini kazi wanazofanya. Akashauri Filikunjombe
Akaongeza kuwa hata
wakiwapa shilingi elfu tano ataona tu umemtambua na siyo hao tu kuna wazee
ambao wanalipwa pensheni baada ya kustaafu serikalini lakini wapo wazee wale
ambao walikuwa wakifanya kazi katika sekta zisizo rasmi.
‘’’’ sisi tumekwenda
zaidi ya hapo tumesema si hao wenyeviti tu wanaostahili kulipwa, kuna wazee
wanaopata pesheni kwa sababu walikuwa watumishi wakastaafu, lakini tumesema
hapana mtu yeyote ambaye saa hizi ni mzee iwe alikuwa sekta isiyorasmi au rasmi
maana yake ametumia nguvu zake katika taifa hili akiwa kijana katika kuliendeleza
taifa hili. Akafafanua Mbunge huyo
Filikunjombe akaongeza
kuwa idadi ya wazee nchini inafikia
milioni 4 tu nguvu zao zimetumika kwa hiyo kuna haja ya kuainisha umri wa wazee
hao wanaostahili kupata pesheni hata kama ni shilingi ishirini elfu zinaweza
kuwafariji.
Akatoa mfano kwa rais
robert mgambe wa Zimbabwe ambaye amejizolea sifa kwa kuwathamini na kutambua wazee
lakini watu wake walikuwa wanasoma bure kwa hiyo leo hii ukisema lolote juu
yake wananchi wanatambua jitihada zake.
Wenyeviti wa vijiji
hawatakiwi kuacha kazi yao kwa sababu kazi hiyo waliomba kwa kugombea kwa hiyo
watakapofanya tofauti watakuwa hawajatenda haki kwa serikali na kwa wale
waliowachagua.
mwisho
No comments:
Post a Comment