Na
Bazil Makungu Ludewa
WAKATI
serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikitafakari na kutafuta
namna ya kuwakopesha madiwani usafiri kama ilivyo kwa wabunge, mbunge
wa Jimbo la Ludewa katika Mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe ametoa
jumla ya pikipiki mpya 34 kwa madiwani wote wa Halmashauri ya wilaya
ya Ludewa bila kujali itikadi zao kisiasa ili kuwarahisishia kutoa
huduma kwa wananchi jimboni mwake.
Filikunjombe
ametoa pikipiki hizo kwa madiwani 25 wa majimbo miongoni mwao wawili
ni kutoka vyama vya chadema na Nccr mageuzi na madiwani 9 wa viti
maalum pamoja na mipira mitano mitano kwa kila diwani ili kuboresha
michezo kwa kila kata pamoja na kuwafanya vijana kupenda michezo
badala ya kujihusisha na ngono.
Akikabidhi
pikipiki kwa madiwani hao mtendaji na katibu wa mbunge wa Ludewa
Stanley Gowele alisema mbunge ametekeleza ahadi yake aliyowaahidi
madiwani wake miaka miwili iliyopita kama njia ya kuwafikia wananchi
kirahisi.
“” pikipiki
hizi najua zitaongeza ajira kwa vijana, zitaingizia halmashauri
mapato na mbali ya kuwarahisishia madiwani kufanyakazi zao pia
zitawaingizia vipato wao wenyewe kwa kutokana na serikali kuruhusu
bodaboda kubeba abilia.”” alisema Gowele
Wakizungumza
na gazeti hili kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema saa ya
ukombozi ni sasa kwani jiografia mbaya ya wilaya ya Ludewa iliyojaa
milima imekuwa ikiwapa wakati mgumu wa kuyafikia maeneo yao ya
uwakilishi lakini kwa sasa pikipiki zitawarahisishia kufanyakazi zao.
Kwa upande
wake diwani mkongwe kutoka kata ya Ibumi Edward Haule alisema
kutekelezwa kwa ahadi ya mbunge kuwaletea madiwani usafiri wa
pikipiki kutarahisha utendaji wa kazi na kuwafikia wananchi kwa
wakati hasa ukilinganisha na jiografia ngumu ya miundombinu ya
barabara wilayani Ludewa.
Kwa mujibu
wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika Agost 2012 wilaya ya Ludewa
inajumla ya wakazi 128,155 kati yao wanaume ni 60,477 na wanawake
67,678 wastani wa ongezeko la watu kwa mwaka ni 1.6% hadi kufikia
2012 na sasa wilaya ya Ludewa inakadiriwa kuwa na watu 152, 285 kati
yao wanawake 79,318 na wanaume ni 72,968 ambapo kiutawala wilaya ya
Ludewa imegawanyika katika tarafa 5 kata 25 vijiji vilivyoandikishwa
77 na vitongoji 340.
Wilaya ya
Ludewa ina eneo la kilomita za mraba 8,397 kati ya hizo kilomita za
mraba 73.54 ni hifadhi ya misitu, kilomita za mraba 2,072 ni maji na
milima na kilomita 6,251.46 zinafaa kwa makazi ya watu na kilimo.
mwisho
No comments:
Post a Comment