Na Bazil Makungu Ludewa
MKUU
wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha amewata Madiwani katika halmashauri hiyo kuanza
mpango wa kuhakikisha kila tarafa inakuwa na shule ya sekondari moja yenye
yenye kidato cha tano na sita na majengo kwa ajili ya maabara za phizikia,kemia
na baolojia.
Agizo
hilo alilitoa jana katika ufunguzi wa kikao cha kawaida cha baraza kuu la
madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa kilichofanyika kwenye ukumbi wa
halmashauri hiyo alipoalikwa kama mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine
Madaha aliwataka madiwani na watendaji kusimamia vizuri miradi ya maendeleo
katika maeneo yao.
Mkuu
wa wilaya ya Ludewa amefikia hatua hiyo ya kuhakikisha kila tarafa inakuwa na
sekondari ya kidato cha tano na sita kutokana na wilaya yake kuwa na sekondari
moja tu ya Ulayasi iliyopo katika kata ya Mlangali yenye kidato cha tano nasita
kati ya sekondari 22 zilizopo katika wilaya hiyo.
Aidha
Madaha amekemea vikali tabia ya wananchi wilayani Ludewa kuacha mifugo ikizagaa
No comments:
Post a Comment