Saturday, November 16, 2013

MAJI YAWE WANANCHI LUDEWA WAKAA SIKU MBILI BILA KUOGA ILI ZE KUMTOSHA RAIS JAKAYA KIKWETE





                                  Na Bazil Makungu Ludewa


 WANANCHI Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wamekaa kwa muda wa siku mbili mfululizo bila kuoga ili maji  yaliyopo ili yatoshe kumhudumia rais  Dr Jakaya Kikwete na msafara wake kutokana na mji wa Ludewa kukabiliwa na uhaba wa maji kwa muda mrefu sasa.

Akitoa taarifa  mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe alimwambia rais kuwa yeye na wananchi wanaoishi katika makao makuu ya wilaya ya Ludewa wamekaa siku mbili mfululizo bila kuoga ili kupisha wageni walioongozana  na rais wapate maji bila kubughudhiwa hii ni kwa mujibu wa mila na desturi la kabila wa wapangwa.

Mji wa Ludewa unakabiliwa na uhaba wa maji kwa muda mrefu sasa ambapo wananchi hao wanalazimika kutumia maji yasiyosalama kutoka katika mto Lingalangala na chemichemi za  bonde la kigaye ambapo akina mama hulazimika kuamka usiku wa manane kupanga foleni kusubiria maji hayo.

‘’’’ mheshimiwa Rais mimi sijaoga siku mbili na hata wananchi waliopo hapa hawajagusa maji ili rais wao upate maji yakukutosha, tunayo mito na maji kule milimani lakini hakuna maji tunaomba kauli yako ya uhakika.’’’’ alisema Filikunjombe

Kwa upande wake naibu waziri wa maji Dr Binilithi Mahenge aliwahakikishia wananchi wa Ludewa kuwa serikali imejipanga kukabiliana na uhaba wa maji mjini ambapo alisema jumla ya shilingi b. 2.4 zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2013/14 kwa ajili ya Ludewa.

Mahenge aliongeza kuwa jumla ya shiling m.74 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu chakavu katika mji wa Ludewa na kutaja chanzo kingine cha maji cha Mapetu kuwa kimetengewa jumla ya shilingi m.300 ambapo mtego huo utakuwa km 5 na kutoa lita 345 kwa siku.

Hata hivyo waziri Mahenge alimtupia lawama mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya Ludewa na mhandisi wa maji wilaya wilaya hiyo kutokana na uzembe wao wa kutofika Arusha kupata maelekezo na kutangaza tenda za miradi ya maji.

Rais Kikwete anamalizia ziara yake katika wilaya ya Ludewa ingawa ni ukamilishaji wa ziara yake katika mkoa wa Njombe leo ambapo kesho atakuwa na mkutano wa majumuisho baada ya kuzindua mkoa huo.

                                  mwisho


No comments:

Post a Comment