Saturday, November 16, 2013

TANZANIA INAONGOZA KWA KUWA NA AINA MBALIMBALI ZA MADINI LAKINI HAINA MADINI JOTO. Na Bazil Makungu Ludewa WANANCHI wametakiwa kukabiliana na magonjwa yanayotokana na upungufu wa madini joto mwilini kwa kudai na kununua chumvi yenye madini joto ya kutosha ili kukabili tatizo hilo linaloathiri afya na maendeleo ya jamii pamoja na kushuka kwa uzalishaji mali na uchumi. Takwimu hizo zilitolewa jana na taasisi ya chakula na lishe nchini kwenye semina ya siku moja kwa wadau mbalimbali iliyofanyika wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambapo ilionesha kuwa madini hayo huagizwa nje ya nchi kutokana na Tanzania kukosa kabisa madini hayo muhimu. Akizungumza katika semina hiyo Eloy Sigara mwezeshaji kutoka taasisi ya chakula na lishe Tanzania alisema kutokana na madini joto kuagizwa ndiyo maana kilogram moja nchini huuzwa kwa shilingi 95,000 jambo linalopelekea watengenezaji wa bidhaa hiyo muhimu kushindwa kumudu bei na kuamua kutengeneza na kuuza chumvi isiyo na madini joto ya kutosha. ‘’’’’ tatizo la upungufu wa madini joto hapa Tanzania ni la tatu kwa ukubwa katika matatizo ya lishe likitanguliwa na tatizo la nishati na upungufu wa akili na mkoa wa njombe unakabiliwa na tatizo kubwa hivyo kila kaya inatakiwa kupata chumvi yenye madini joto ya kutosha’’’’ alisema Sigala Naye bi Vumilia Lyatuu kwa upande wake akawataka washiriki wa semina hiyo hasa maafisa wa afya wilaya, kata na vijiji kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari zinazotokana na ukosefu wa wa madini hayo hususani akina mama wajawazito kuwa ni pamoja na mimba kuharibika, mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake au kuzaliwa mfu, kuzaliwa na mtindio wa ubongo na kuchelewa kubarehe, udumavu wa ubongo na mwili,kuzaliwa na ulemavu wa viungo na kadharika. Lyatuu alisema utafiti wa awali uliofanyika mwaka 1980 takwimu zilionesha kuwa asilimia 40 ya watanzania walikiri kuishi kwenye maeneo yenye upungufu wa madini joto ambapo asilimia 25 ya watanzania walikuwa wameathirika na uvimbe wa tezi la shingo(goitre). Aliitaja mikakati ya serikali kuwa ni pamoja na kuagiza mashine na vifaa vya kuchanganya chumvi na madini joto, utoaji wa madini joto ya nyongeza na vidonge vyenye madini joto, kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kwa kutumia njia ya radio, magazeti na television, kuanzishwa kwa sheria ya chumvi,kuwaunganisha wazalishaji chumvi na wadau wengine nchini. Mikakati mingine ni kuweka mfumo wa ufuatiliaji, kuwepo na kamati ya kitaifa inayoratibu mpango wa kudhibiti upungufu wa madini joto kwa kuwa na wajumbe kutoka wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya afya, madini,fedha, na viwanda na biashara. Hata hivyo changamoto zinazoikabili taasisi ya chakula na lishe ni pamoja na wazalishaji kutofuata vigezo vya uzalishaji bora wa chumvi yenye madini joto, viwango vya madini joto, usafi na uhifadhi, uwepo wa wazalishaji wadogo wengi wa chumvi waliotawanyika katika maeneo tofauti, kutokuwepo na upatikanaji endelevu wa madini joto na mapungufu katika mfumo wa usambazaji. Ni kutokana na changamoto hizo maafisa afya katika ngazi za wilaya, kata na vijiji wilayani Ludewa walipitisha maazimio katika maeneo yao na kuhakikisha jamii inatumia chumvi yenye madini joto ya kutosha, kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi ya chumvi yenye madini joto, kuhamasisha jamii juu ya utunzaji chumvi, sheria ya chumvi, kuingiza haraka kwenye kamati za maendeleo za kata, kupima ubora wa chumvi katika ngazi ya kaya na suala la chumvi yenye madini kuwa suala la mtambuka na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kila baada ya robo mwaka. mwisho



 ELOY SIGARA MWEZESHAJI KUTOKA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE DAR ES SALAAM AKITOA SEMINA KWA MAAFISA AFYA WILAYA YA LUDEWA NA WADAU WA CHUMVI
 VUMILIA LYATUU KUTOKA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TAIFA AKITOA MADA KWA WASHIRIKI WA SEMINA YA MATUMIZI YA CHUMVI YENYE MADINI JOTO YA KUTOSHA
 AFISA AFYA WILAYA YA LUDEWA KELVIN MFUSE WA KWANZA KULIA NA MWENZAKE WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA SEMINA HIYO
 WAFANYABIASHARA YA CHUMVI WAKIPATA SEMINA KUHUSA UTUNZAJI WA CHUMVI KABLA HAIJAFIKA KWA MLAJI




 CASTORI KIBASSA AFISA AFYA AKIONESHA KWA WASHIRIKI KIFAA CHA KUPIMIA CHUMVI

 CHUMA CHA LIGANGA
 KIJIJI CHA AMANI AMBACHO KIPO KATIKA ORODHA YA VIJIJI VINAVYOTARAJIA KUHAMA KUPISHA MGODI
 SAMAKI WA ZIWA NYASA AINA YA MBUFU WAKIWA SOKONI SAMAKI MMOJA ANAUZWA KWA YA SHILINGI 5000

WANANCHI WENGI NCHINI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU MATUMIZI YA  CHUMVI YENYE MADINI JOTO YA KUTOSHA

WANANCHI wametakiwa kukabiliana na magonjwa yanayotokana na upungufu wa madini joto mwilini kwa kudai na kununua chumvi yenye madini joto ya kutosha ili kukabili tatizo hilo linaloathiri afya na maendeleo ya jamii pamoja na kushuka kwa uzalishaji mali na uchumi.

Takwimu hizo zilitolewa jana na taasisi ya chakula na lishe nchini kwenye semina ya siku moja kwa wadau mbalimbali iliyofanyika wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambapo ilionesha kuwa madini hayo huagizwa nje ya nchi kutokana na Tanzania kukosa kabisa madini hayo muhimu.

Akizungumza katika semina hiyo Eloy Sigara mwezeshaji kutoka taasisi ya chakula na lishe Tanzania alisema kutokana na madini joto kuagizwa ndiyo maana kilogram moja nchini huuzwa kwa shilingi 95,000 jambo linalopelekea watengenezaji wa bidhaa hiyo muhimu kushindwa kumudu bei na kuamua kutengeneza na kuuza chumvi isiyo na madini joto ya kutosha.

‘’’’’ tatizo la upungufu wa madini joto hapa Tanzania ni la tatu kwa ukubwa katika matatizo ya lishe likitanguliwa na tatizo la nishati na upungufu wa akili na mkoa wa njombe unakabiliwa na tatizo kubwa hivyo kila kaya inatakiwa kupata chumvi yenye madini joto ya kutosha’’’’ alisema Sigala

Naye bi Vumilia Lyatuu kwa upande wake akawataka washiriki wa semina hiyo hasa maafisa wa afya wilaya, kata na vijiji kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari zinazotokana na ukosefu wa wa madini hayo hususani akina mama wajawazito kuwa ni pamoja na mimba kuharibika, mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake au kuzaliwa mfu, kuzaliwa na mtindio wa ubongo na kuchelewa kubarehe, udumavu wa ubongo na mwili,kuzaliwa na  ulemavu wa viungo na kadharika.

Lyatuu alisema utafiti wa awali uliofanyika mwaka 1980 takwimu zilionesha kuwa asilimia 40 ya watanzania walikiri kuishi kwenye maeneo yenye upungufu wa madini joto ambapo asilimia 25 ya watanzania walikuwa wameathirika  na uvimbe wa tezi la shingo(goitre).

Aliitaja mikakati ya serikali kuwa ni pamoja na kuagiza mashine na vifaa vya kuchanganya chumvi na madini joto, utoaji wa madini joto ya nyongeza na vidonge vyenye madini joto, kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kwa kutumia njia ya radio, magazeti na television, kuanzishwa kwa sheria ya chumvi,kuwaunganisha wazalishaji chumvi na wadau wengine nchini.

Mikakati mingine ni kuweka mfumo wa ufuatiliaji, kuwepo na kamati ya kitaifa inayoratibu mpango wa kudhibiti upungufu wa madini joto kwa kuwa na wajumbe kutoka wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya afya, madini,fedha, na viwanda na biashara.

Hata hivyo changamoto zinazoikabili taasisi ya chakula na lishe  ni pamoja na wazalishaji kutofuata vigezo vya uzalishaji bora wa chumvi yenye madini joto, viwango vya madini joto, usafi na uhifadhi, uwepo wa wazalishaji wadogo wengi wa chumvi waliotawanyika katika maeneo tofauti, kutokuwepo na upatikanaji endelevu wa madini joto na mapungufu katika mfumo wa usambazaji.

Ni kutokana na changamoto hizo maafisa afya katika ngazi za wilaya, kata na vijiji wilayani Ludewa walipitisha maazimio katika maeneo yao na kuhakikisha jamii inatumia chumvi yenye madini joto ya kutosha, kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi ya chumvi yenye madini joto, kuhamasisha jamii juu ya utunzaji chumvi, sheria ya chumvi, kuingiza haraka kwenye kamati za maendeleo za kata, kupima ubora wa chumvi katika ngazi ya kaya na suala la chumvi yenye madini kuwa suala la mtambuka na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kila baada ya robo mwaka.

                               mwisho


No comments:

Post a Comment