Na Bazi
Makungu Ludewa
MBUNGE wa jimbo la Ludewa katika Mkoa wa Njombe Deo
Filikunjombe amefanikiwa kuchangisha papohapo jumla ya shilingi m.30.7 kati ya shilingi
m.90 zinazotakiwa na kusakwa na waumini wa kanisa katoliki kwa ajili ya ununuzi
wa gari la parokia ya Ludewa mjini.
Harambee hiyo ilifanyika machi mwaka huu katika kanisa la
yesu kristu mkombozi lililopo Ludewa mjini ambapo ilifanyika misa maalumu kwa
kuwashirikisha waumini kutoka vigango vyote vinyounda parokia hiyo ambavyo ni
pamoja na Nyamapinda, Ludewa(K) na Ngalawale.
Ujio wa mbunge huyo ulikuja kufuatia mwaliko wa kamati ya
ununuzi wa gari ambayo ilimtuma diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchiro na
mwenyekiti wa kamati hiyo mzee Kayombo kumwomba Filikunjombe kuja kuendesha
harambee hiyo.
No comments:
Post a Comment