AFISA
MTENDAJI ATAFUNA PESA YA MRADI WA MAJI
.ashindwa
kulipa nyumba yake yapigwa mnada na balaza la kata
Na
Charles Mhagama Ugela Mkongobaki
AFISA
mtendaji wa kijiji cha Ugela kata ya mkongobaki tarafa ya Liganga
Ludewa katika Mkoa wa Njombe Xavery Haule amalazimika kuiacha nyumba
na kujisitili kwa majirani baada ya balaza la kata kuiuza nyumba yake
kutokana na kesi ya kutafuna bila huruma jumla ya shilingi 230,000 za
mradi wa maji katika kijiji hicho.
Tukio
la kuuzwa kwa nyumba ya mtumishi huyo wa umma lilifanywa na balaza
la kata ya Mkongobaki Aprili 23 mwaka huu baada ya mshtakiwa
kushindwa kulipa pesa hiyo ya kijiji kwa awamu kama alivyoahidi
alipokabidhi nyumba kama dhamana yake.
Akizungumza
na gazeti hili John Mhagama ambaye ni karani wa balaza hilo alikiri
kuwepo kwa kesi hiyo na kuongeza kuwa balaza limelazimika kuuza
nyumba ya Bw Xavery Haule baada ya kushindwa kutekeleza ahadi yake ya
kulipa pesa kwa awamu kama alivyoomba.
‘’’’’’
wananchi
wa kijiji cha ugela walibuni mradi wa maji na kuamua kuchanga kila
kaya na zikapatikana jumla ya shilingi 230,000 kwa ajili ya kujenga
tanki la maji lakini afisa huyo akaziweka mfukoni na alipoitwa kwenye
kamati ya maendeleo la kata (KAMAKA) alikiri na kuamuriwa kulipa
polepole kwa awamu aliposhindwa kulipa kesi ilipelekwa balaza la
kata.’’’ alisema mhagama
Kwa
upande wake afisa mtendaji Exavery Haule alipoulizwa na gazeti hili
kuhusu tuhuma na hukumu aliyopata alikiri kukusanya fedha 230,000 kwa
ajili ya mradi wa maji kutoka kwa wenyeviti wa vitongoji vya Kigina
na Mlangali ndani na kuongeza kuwa hakustahili kupewa hukumu hiyo kwa
sababu fedha ilifanya kazi halali na mwenyekiti anatambua.
‘’’’’
nimesikitishwa
na hukumu iliyotolewa na balaza la kata kwa sababu pesa hiyo
sikutumia kwa manufaa yangu bali zilitumika kwa shughuli halali ya
kupokea wageni na wafadhili toka Hispania waliofika kuangalia mradi
wa maji na nilikubaliana na mwenyekiti.’’’’ alisema Xavery
Akifafanua
matumizi ya fedha hiyo Haule sh105,000 zilitumika kununua kuku 6 kama
kitoweo cha wageni, sh12,000 mchele kg 5, sh45,000 soda creti 3,
sh10,000 ulanzi lita 40, sh16,000 pombe lita 40, sh14,400 maji ya
kunywa, sh15,000 nyama kg 2 na viungo, sh5000 debe la viazi, sh 8000
mafuta ya kupilia, sh 9000 vikapu kwa ajili ya zawadi ya wageni.
Vingine
ni sh 6000 nyungo kwa ajili ya zawadi ya wageni, sh2,600 viungo na
mboga za majani, sh5000 vocha, 5000 alimpa mwenyekiti wa kijiji.
MWISHO
No comments:
Post a Comment