Thursday, May 8, 2014


WATANZANIA WAMETAKIWA KUANDIKA VIJALIDA ILI KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUSOMA VITABU ILI KWENDA NA WAKATI.

. Asema ukitaka kumnyima mtanzania pesa weka ndani ya kitabu.

Na Bazil Makungu

ASKOFU Mstaafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Doyasisi ya kusini kati Wilayani Makete katika Mkoa wa Njombe dakta Solomon Swallo amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kusoma na kuandika vitabu katika maisha yao ya kila siku ili kujitunzia kumbukumbu na kupanua uelewa katika mambo mbalimbali.

Askofu Swallo aliyasema hayo hivi karibuni katika kanisa hilo usharika wa Bulongwa alipotunukiwa shahada ya uzamivu (PHD) na chuo cha nchini marekani ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa akisherekea miaka themanini na moja(81) tangu kuzaliwa kwake.

Askofu Swalo aliyelitukia kanisa kwa miaka 24 akiwa askofu wa doyasisi ya kusini alionesha kusikitishwa kwake na tabia ya watanzania wengi kupenda mambo ya starehe na burudani mbalimbali huku wakiweka pembeni suala muhimu la uandishi na usomaji wa vitabu.

“”” ndugu zangu watanzania ninyi ni watu wa ajabu sana nashangaa kuona watu wanaweza kukaa wiki nzima hata mwezi hajasoma kitabu chochote, ukitaka kumnyima pesa mtanzania weka katika kitabu utazikuta zikiwa salama kwa sababu hawana utamaduni wa kusoma vitabu.””” alionesha maskitiko askofu Swallo

Kutokana na uvivu huo Swallo amewataka watanzania wote kujizoeza kuandika masuala ya kawaida na kutunza kumbukumbu hata katika vijarida vyenye kurasa chache zenye kuelezea matukio mbalimbali yakiwemo mambo yanayotokea kila siku katika jamii zao bila kusubiri matukio makubwa.

mwisho

No comments:

Post a Comment