MAFURIKO MTO
LUHUHU YAHARIBU MAZAO HEKTA 126 ZA MPUNGA ZAMEZWA NA MAJI.
Na
George Ngalawa Manda
WANANCHI
wanaoishi kwenye vijiji vilivyopo kata za Luhuhu na Manda katika
tarafa ya Masasi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wamo hatarini
kukosa chakula mwaka huu kutokana na mto Luhuhu kujaa maji kufuatia
mvua kubwa inayoendelea na kudumu zaidi ya mwezi sasa.
Wakulima
walioathirika na mafuriko hayo ni pamoja na wale wanaolima mashamba
ya mihogo na mpunga katika vijiji vya Ngelenge, Kipingu, Ilela,
Nsungu na Fokland ambao sasa wamelazimika kuhama makazi yao kutokana
na maji kujaa katika nyumba zao.
Afisa kilimo
na mifugo Faraja Mpunga akitoa takwimu alisema kufuatia mafuriko hayo
hekta 126 za mpunga zimemezwa na maji, hekta 29 za mihogo na mahindi
hekta 28.25 na kuongeza kuwa mafuriko hayo yanatokana na mvua kubwa
iliyonyesha machi 31 mwaka huu.
Akizungumza
na radio uplands afisa mtendaji wa kata ya Luhuhu Musa Kazimoto
alisema mafuriko hayo yalianza machi 31 mwaka huu katika mashamba ya
wananchi ambapo tangu wakati huo mpaka sasa mazao yamefunukwa na
maji.
Kazimoto
alisema kufuatia mafuriko hayo ofisi yake imetoa taarifa katika ngazi
vikiwemo vyombo vya serikali lakini wamekuwa wakifiki na kuondoka
kufuatia hali hiyo serikali za vijiji zimetoa maelekezo kwa wananchi
ili waanza kuondoa mazao ambayo yanaweza kuokolewa kwa kutumia
mitumbwi.
WATUMISHI
WAMLAUMU MKURUGENZI WAO MEI MOSI.
.Sherehe
ilipelekwa kijijini kwao lakini zawadi zikarudi mjini
Na
Enhard Mwachiro Lugarawa
WATUMISHI
na wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa katika mkoa wa
Njombe waliopo vijijini wamemlalamikia mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya hiyo kwa kutokutenda haki katika utoaji zawadi kwa wafanyakazi
bora katika sherehe za mei mosi mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwenye
kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (mei mosi) iliyofanyika
kiwilaya katika kijiji cha Lugarawa tarafa ya Liganga ambapo mgeni
rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha.
Wakizungumza
na gazeti hili kwa nyakati tofauti wafanyakazi hao walisema sherehe
hizi kiwilaya zimefanyika kama maigizo kwamba pamoja na changamoto
walizonazo za kufanyakazi katika mazingira magumu wanakatishwa tamaa
na mwajiri wao kutokana na kutoa zawadi na wafanyakazi bora kwa
upendeleo.
‘’’’’ zaidi
ya asilimia 80 ya wafanyakazi waliopata zawadi za ufanyakazi bora
mwaka huu walitoka nao mjini kuja kufanya maigizo huku Lugarawa
lakini mbaya zaidi wengine tumeshuhudia wakipata zawadi hizo kila
mwaka kuna nini? Aliuza mwalimu mmoja ambaye hakutaka jina lake
liandikwe
Wamesema
hakuna sababu ya kupeleka sherehe za mei mosi katika maeneo ya
vijijini wakati wanaonufaika ni wafanyakazi wa mjini. ‘’’’’
tunamwomba mkurugenzi aache kutudhihaki kama siku nyingine afanye
sherehe hizo karibu na watu wake anaopendelea kuwapa zawadi za
ufanyakazi bora.’’’’ alilalamika muuguzi mmoja
Aidha
katika risala yao kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Ludewa
wafanyakazi katika halmashauri hiyo wametaja shinikizo la damu kama
chanzo cha vifo kwa watumishi wengi wilayani humo.
Akisoma
risala ya wafanyakazi mbele ya mgeni rasmi katibu mkuu wa shirikisho
la vyama huru vya wafanyakazi wilaya ya Ludewa Joseph Mvanga alisema
wafanyakazi wamekuwa wakipoteza maisha kwa magonjwa mbalimbali lakini
kubwa ikiwa shinikizo la damu kutokana na kudai mafao yao bila
mafanikio, kutopandishwa mishahara na vyeo.
Mvanga
alisema mwajiri amekuwa na kiburi na kuvaa miwani ya mbao kama vile
haoni matatizo ya watumishi wake huku akiziba masikio kwa pamba kama
vile hasikii kelele na kilio cha watumishi wake jambo linalopelekea
wafanyakazi kufa kwa mawazo na maisha magumu.
Akijibu
risala hiyo mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha aliwaondoa hofu
watumishi na wafanyakazi katika halmashauri ya wilaya kwa kuwaambia
kuwa madai yao yatashughulikiwa.
No comments:
Post a Comment