Tuesday, June 3, 2014

MAUAJI YA KIKATIRI MKOA WA NJOMBE, LUDEWA YAONGOZA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA, WATOTO WADOGO WARITHISHWA UCHAWI BADALA YA ELIMU. .Ngonyani awataka wananchi kushirikiana na polisi na kuhakikisha kila familia haina mhalifu Na Bazil Makungu WILAYA ya Ludewa imetajwa kuwa kinara wa matukio ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina katika mkoa wa njombe huku watoto wadogo wakirithishwa uchawi badala ya kupelekwa shule kupata elimu wakati huo mkoa wa njombe ukitajwa kushika nafasi ya pili kitaifa baada ya mkoa wa geita kushikilia nafasi ya kwanza. Akizungumza hivi karibuni na viongozi wa dini,maafisa tarafa, maafisa watendaji kata na vijiji, wafanyabiashara, wadau mbalimbali na watu maarufu wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe kamanda wa polisi kamishna msaidizi mwandamizi Fulgence Ngonyani alisema kumekuwa na upungufu wa mahusiano duni kati ya wananchi na polisi jambo linalopelekea jamii kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo. Ngonyani aliwaeleza wananchi kuwa jeshi la polisi peke yake haliwezi kumaliza uhalifu unaotokea katika jamii lakini kama wananchi watachukia uhalifu na kuamua kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa sahihi na pengine kuwakamata wahalifu ‘’’ inawezekana kabisa kupunguza uhalifu kwa sababu wahalifu wote wanatoka katika familia zetu tunaishi nao tunakula nao tunalala nao tunawafahamu tuhakikishe na kuona ndani ya familia zetu hakuna mhalifu.’’’’ alisisitiza ngonyani TAKWIMU Hadi sasa sensa ya watu na makazi inaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya watu milioni 44,932,000 idadi ya vitongoji ikifikia 60,359, vijiji 11,137 kata 3,335 huku idadi ya wilaya ikiwa 151 lakini askari polisi nchi nzima ni 41,416 kati yao wamo maofisa na vikosi mbalimbali wakiwemo wagonjwa pia hata hivyo idadi ya vituo vya polisi ni 868 vituo vidogo vya polisi 501 kwa hiyo ukiangalia idadi ya vitongoji, vijiji, kata na wilaya ni kubwa kuliko idadi ya askari waliopo.













No comments:

Post a Comment