.Ngonyani awataka
wananchi kushirikiana na polisi na kuhakikisha kila familia haina
mhalifu
Na Bazil Makungu
WILAYA ya Ludewa imetajwa
kuwa kinara wa matukio ya mauaji yanayohusishwa na imani za
kishirikina katika mkoa wa njombe huku watoto wadogo wakirithishwa
uchawi badala ya kupelekwa shule kupata elimu wakati huo mkoa wa
njombe ukitajwa kushika nafasi ya pili kitaifa baada ya mkoa wa geita
kushikilia nafasi ya kwanza.
Akizungumza hivi karibuni
na viongozi wa dini,maafisa tarafa, maafisa watendaji kata na vijiji,
wafanyabiashara, wadau mbalimbali na watu maarufu wilayani Ludewa
katika Mkoa wa Njombe kamanda wa polisi kamishna msaidizi mwandamizi
Fulgence Ngonyani alisema kumekuwa na upungufu wa mahusiano duni kati
ya wananchi na polisi jambo linalopelekea jamii kushindwa kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo.
Ngonyani aliwaeleza
wananchi kuwa jeshi la polisi peke yake haliwezi kumaliza uhalifu
unaotokea katika jamii lakini kama wananchi watachukia uhalifu na
kuamua kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa sahihi na pengine
kuwakamata wahalifu ‘’’ inawezekana kabisa kupunguza uhalifu
kwa sababu wahalifu wote wanatoka katika familia zetu tunaishi nao
tunakula nao tunalala nao tunawafahamu tuhakikishe na kuona ndani ya
familia zetu hakuna mhalifu.’’’’ alisisitiza ngonyani
TAKWIMU
Hadi sasa sensa ya watu
na makazi inaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya watu milioni
44,932,000 idadi ya vitongoji ikifikia 60,359, vijiji 11,137 kata
3,335 huku idadi ya wilaya ikiwa 151 lakini askari polisi nchi nzima
ni 41,416 kati yao wamo maofisa na vikosi mbalimbali wakiwemo
wagonjwa pia hata hivyo idadi ya vituo vya polisi ni 868 vituo vidogo
vya polisi 501 kwa hiyo ukiangalia idadi ya vitongoji, vijiji, kata
na wilaya ni kubwa kuliko idadi ya askari waliopo.
JESHI LA POLISI NJOMBE
Idadi ya askari polisi
katika mkoa wa njombe ni 571 tu wakati mkoa unazo kata 96, tarafa 18
hata hivyo miongoni mwao kuna mgawanyo wa shughuli mbalimbali kama
mahakamani, wamo pia maafisa na wagonjwa aidha nguvu kazi ya polisi
inazidi kupungua kama idara zingine kwa vifo vya watumishi kwa hiyo
ipo haja ya kila mmoja kuwa mlinzi kwa kushirikiana na jeshi la
polisi ili kupata usalama kwani ulinzi shirikishi ni kusaidia,
kupeana taarifa za uhalifu na ulinzi jiani kwa sababu mtu anaweza
kuchagua rafiki lakini hawezi kuchagua jirani.
’’’’ kuna mauaji
yanatokea katika maeneo yetu na mkoa wa njombe ndio unaongoza kwa
mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na katika kipindi cha
mwaka jana matukio 18 ya mauaji ya kikatili yalitokea katika mkoa
huu.’’’’ aliongeza kamanda Ngonyani
OCD LUDEWA
Akitoa taarifa mkuu wa
polisi wilaya ya Ludewa mrakibu wa polisi Gali la moshi alisema
katika kipindi cha mwaka wa 2006 hadi 2011 kesi 31 za mauaji
ziliripotiwa ofisini kwake mwaka 2012 matukio makubwa 72 yaliripotiwa
huku mauaji yakifikia 17, mwaka 2013 makosa makubwa yalikuwa 64
mauaji yakiwa 15 na mwaka 2014 mauaji yanayotokana na imani za
kishirikina hadi machi yapo 8,
Wakitoa ushauri kwa jeshi
la polisi washiriki wa mikutano walisema kuna haja ya kuwatambua
waganga wa tiba ya asili na kuzungumza nao juu ya ushiriki wao katika
mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina kwa kuagua jambo ambalo
ni kinyume na vibali vyao .””” kila kijiji, kata, na tarafa
iwatambue waganga wa jadi na kuwaorodhesha kisha kufanya nao kikao na
kupewa miiko katika utendaji wao wa kazi.’’’’ aliagiza gali
la moshi
Mambo mengine yaliyotajwa
kusababisha mauaji wilayani Ludewa ni pamoja na ulevi wa ulanzi, wivu
wa mapenzi. Wazee wametakiwa kuacha maramoja tabia ya kuwarithisha
watoto wadogo uchawi badala yake wawarithishe elimu ambayo itakuwa ni
ukombozi katika maisha yao lakini uchawi hauna faida faida kwa mtoto
zaidi ya kupandikiza roho mbaya, chuki na fitina moyoni mwake.
USALAMA KATIKA NYUMBA ZA
IBADA
Viongozi wa dini wanayo
nafasi kubwa ya kukomesha uhalifu katika maeneo yetu kwa sababu
baadhi ya wahalifu wamo ndani ya makanisa na misikiti wanayoiongoza
hivyo wanaweza kukomesha kwa kuwahubiria na kuwaeleza madhara ya
uhalifu na wakaongoka. aidha viongozi wa dini wametakiwa kuanzisha
kamati za ulinzi na usalama kamati nyumba zao za ibada ili kutambua
mienendo ya watu wasokuwa waumini wa makanisa na misikiti yao.
MAAFISA WATENDAJI
Wametakiwa kurejesha na
kuanzisha madaftari ya wakazi ili kujua idadi ya watu wanaoishi
katika maeneo yao lakini pia itakuwa rahisi kubaini na kutambua
wageni wanaoingia katika mitaa yao hata hivyo kutambua wageni
wavamizi wa ardhi wanaoleta kero na migogoro isiyokuwa ya lazima
ndani ya jamii na maeneo yao.
No comments:
Post a Comment