Na Bazil Makungu
Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
Imewataka wanahabari Kuendelea Kusema Ukweli juu ya Vyakula Madawa
Feki ambayo yamekuwa Yakiendelea Kusambazwa Kwa Wananchi Ili Kulinda
Afya za Walaji.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mwanasheria wa
Mamlaka Hiyo Bwana Iskari Fute Wakati Akitoa Semina ya Siku moja kwa
Wahariri na Waandishi wa Habari wa Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika
Jijini Mbeya.
Awali akifungua Semina hiyo Kwa niaba
ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bwana
Leonard Magacha Amesema Kuwa Kutokana na Jamii Kuamini Kila
Kinachotangazwa na Vyombo vya Habari Hivyo Wanahabari Hawanabudi
Kufanya Uchunguzi wa Kina na Kubaini Ukweli wa Kila Habari Kabla ya
Kuitangaza.
Aidha Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
Imefanikiwa Kufungua Ofisi Nyingine Tano Katika Mikoa Tofauti Pamoja
na Kufungua Maabara Kubwa yenye Kiwango cha Kimataifa Kwa ajili ya
Kusogeza huduma karibu na Wananchi badala ya kubaki Dar es salaam.
Akizungumzia suala hili Kaimu
mkurugenzi wa Mamlaka hiyo bwana Chrispin Severe amesema kuwa pamoja
na kufanikiwa kufungua ofisi hizo na Maabara lakini bado mamlaka
imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kupambana na
wafayabiashara wasiowaaminifu.
Amesema matarajio ni kuendelea
kusimamia Viwango vya ubora wa bidhaa,kuwaelimisha wananchi kupitia
waandishi wa Habari hapa Nchini.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa
usalama wa chakula bwana Justin Makisi amesema kuwa endapo mamlaka
hiyo haitosimama vizuri katika kudhibiti matangazo ya biashara ambazo
si halali na hazina ubora basi jamii itapata madhara makubwa na hata
kusababisha vifo kutokana na kutumia madawa na vyakula vilivyokwisha
muda wake.
Amesema kuwa kama mamlaka tayari
imefanikiwa kupiga marufuku na kuyafungia baadhi ya matangazo
yaliyoonekana kupotosha umma ikiwemo dawa ya asili ya Fiterawa
inayodaiwa kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
Katika hatua nyingine amevitaka vyombo
vya habari kutumia nguvu kubwa katika kuendelea kutoa habari na
matangazo yanayopotosha umma katika maeneo mbalimbali ili jamii iweze
kufahamu na kuepukana nayo.
Akizungumzia juu ya kushuka kwa ubora
wa vyakula na Dawa mkurugenzi mkuu wa Maabara Bi.Charys Ugullum
amesema kuwa kama maabara imekuwa ikifanya uchunguzi wa chakula,dawa
na vidozi ili kubaini ubora na usalama wa bidhaa husika ili ziweze
kuingizwa sokoni.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo
ukishafanyika unasaidia katika utoaji wa maamuzi juu ya chakula,dawa
na vipodozi ambavyo vitabainika kuwa vina ubora au havina.
Amesema jumla ya sampuli 7546 za
vyakula zimeshafanyika pamoja na vipodozi tangu kuanzishwa kwa
mamlaka hiyo mnamo mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment