Wednesday, August 6, 2014

FILIKUNJOMBE ATIMUA MKURUGENZI, WAKUU WA IDARA KATIKA MKUTANO WA HADHARA. WANANCHI WAZOMEA NA KUSEMA WANASUBIRI VIFAA VYA ZAHANATI YAO. Na Bazil Makungu Ludewa MBUNGE wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe jana alilazimika kumfukuza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya na wakuu wa idara baada ya kushindwa kutoa maelezo kuhusu vilipo vitanda, magodoro na mashuka vifaa alivyovinunua yeye mwenyewe mwaka mmoja uliopita kwa ajili ya zahanati ya Ihanga iliyopo kata ya Mlangali. Awali Filikunjombe alikataa kufanya mkutano katika uwanja uliokuwa umeandaliwa badala yake akamtaka mwenyekiti wa kijiji cha mlangali ndani kuwaita wananchi na kufungua mkutano kwenye viwanja vya zahanati hiyo Katika ziara yake ya wiki moja ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake Filikunjombe alifuatana na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Horace Kolimba akiwemo kaimu mganga mkuu na wakuu wa idara za kilimo, maji na ujenzi. Hali ya hewa ilianza kuchafuka katika mkutano baada ya Filikunjombe kukagua zahanati na kugundua mapungufu mengi ikiwemo ukosefu wa vitanda vya kupumzikia wagonjwa na akina mama na kitanda cha kujifungulia vifaa ambavyo alivinunua mwenyewe na kutoa fedha ya usafiri na kuikabidhi halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kupeleka katika zahanati lakini wamekaa navyo huku wananchi wakiendelea kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu. Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Horace Kolimba baada ya kukosa majibu alimwomba Filikunjombe ampe wiki moja ili aweze kuvifikisha vifaa hivyo lakini kwa mbunge ilikuwa vigumu kukubali ombi hilo na ndipo hatua ya kuwafukuza ilitimia na kusimamisha mkutano kwa muda mpaka vifaa vyao vitakapoletwa. ‘’’ wananchi mmejionea wenyewe wameshindwa kutoa majibu mbele yenu sasa hatuendelei na mkutano waondoke hapa wakalete vifaa vyetu ndipo mkutano uanze hatuwezi kukaa hapa tunapiga siasa wakati huduma za zahanati zimekaliwa na watendaji, serikali yetu na chama cha mapinduzi inaonekana haifanyikazi kwa sababu ya watendaji wabovu kwenye jimbo langu siwezi kuwavumilia.’’’ alilalamika filikunjombe









































No comments:

Post a Comment