MTOTO Ibrahimu wa Chipungahelo(chips) mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa shule ya msingi Ludewa mjini katika mkoa wa njombe ameuawa na kisha kuliwa/kutafunwa na mbwa wawili vichaa wanaomilikiwa na Bw Bosco Lingalangala mkazi wa Dar es salaam.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna
msaidizi mwandamizi Fulgenzi Ngonjani marehemu pamoja na wenzake walikuwa wakipita njia kwenda kuokota mapera porini kama ilivyo desturi yao lakini lakini mbwa hao wakatokea na kuwavamia.
Ngonyani aliongeza kuwa watoto wengine walifanikiwa kukikimbia na kupotelea porini lakini marehemu katika jitihada za kujikwamua alizidiwa nguvu na mbwa hao ambapo walifanikiwa kumuua na kumla sehemu za siri, mapaja na mgongoni ambapo baada ya polisi na afisa mifugo kufika eneo la tukio walifanikiwa kumuua mbwa mmoja huku mwingine akitokomea kusikojulikana.
Fraja samweli chipungahero taarifa ya kwanza niliambiwa kuwa mwanangu ameumwa na mbwa unatakiwa kulala naye hospitali nikashtuka nilipokwenda nikakuta yupo theata kubwa nilipofika nilikuta mwanangu ameliwa na mbwa. waganga walifanya jitihada za kumuokoa lakini gesi ilikuwa inapitilia.
''' mtoto wangu alizaliwa septemba 21, 2005 inaniuma sana mwanangu kufa kifo kibaya namna hii inasikitisha sana nashindwa kujizuia lakini imetokea sina la kufanya kifo kama hiki kwangu ni mara ya kwanza kushuhudia.'''' alieleza kwa masikitiko makubwa Chips
Wakizungumza na mwandishi wetu Mashuhuda wa tukio hilo mama Haule na mama Kumba ambao ni majirani na wazazi wa mtoto huyo walisema walipofika katika tukio hilo walishindwa kuwasogelea wale mbwa kwa sababu ni wakali sana halafu ni makubwa kiasi hata mtu mzima wangeweza kumdhuru.
''' tulipofika pale kwa sisi wananwake ilikuwa ni vigumu kusogea kutokana na ukubwa na ukali wa mbwa wale tumeshuhudia wakimla mtoto bila huru inasikitisha na ndipo tukakimbilia polisi.''' aliongeza mama Kumba
Naye kaimu afisa mifugo Simoni Haule kwa upande wake alisema kuwa mbwa wale hawajapata chanjo zaidi ya miaka miwili sasa na mwenye mbwa anakaa mjini Dar es salaam kwa hiyo ni jukumu la mmiliki wa mbwa kupelka chanjo.
Haule akaongeza kuwa walipoka eneo la polisi akiwa na askari wa jeshi la polisi alifanikiwa kumuua mbwa mmoja lakini mwingine alitokomea vichakani na juhudi za kumsaka ili kumuua zina endelea na kuwataka watu kuwa makini wasipita vichakani.
mwisho

No comments:
Post a Comment