WAZEE LUDEWA WAENDELEA KUMCHANGIA FILIKUNJOMBE FEDHA ZA KUCHUKULIA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE
Filikunjombe akikabidhiwa fedha na mzee Mwanawalifa za kuchukulia fomu ya kugombea ubunge mwaka 2015 jimbo la Ludewa
Filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilayani Ludewa
Filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilayani Ludewa
Filikunjombe akifurahi na wananchi wa Kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilayani Ludewa hivi karibuni wakati wa mapokezi yake kijijini hapo
Filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilayani Ludewa
Wazee
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameendelea kumchangia mbunge wa jimbo la
Ludewa Mh.Deo.Filikunjombe fedha kwajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge
ili kuendelea kuliongoza jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa nyuma
kimaendeelo.
Akikabidhi
fedha hizo kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa niaba ya mzee wa kijiji cha
Mbwila anayejulikana kwa jina la Mwanawalifa alisema kuwa wilaya ya Ludewa
imekuwa na tabia ya kubadirisha wabunge kila inapofika kipindi cha uchaguzi
kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa wabunge hao lakini kwa sasa
wameridhika na utendaji wa Filikunjombe hivyo hawaoni sababu ya kubadiri
uongozi.
Mzee
Mwanawalifa alisema lutokana na utendaji kazi ukiambatana na umakini wa mbunge
wao wazee wa kata ya Luana wameona ni vyema kumuunga mkono Filikunjombe kwa
kumchangia kiasi kidogo cha fedha ili wakati ukifika achanganye na fedha zake
akachukue fomu ya kugombea ubunge kwani wananchi wa jimbo la Ludewa hawana haja
ya kuwa na Mbunge mwingine zaidi ya Filikunjombe.
Alisema kuwa
chama cha mapinduzi kimekuwa na viongozi wenye uchungu na nchi yao ambao ni
waadirifu na wanaokubalika na wananchi hivyo aliwataka vijana wanaojiunga na
vyama vingine kubaki njia kuu ili kuweza kugombea nafasi mbalimbali ambazo
wataweza kuzitumia vyema kama Filikunjombe ambaye ni mfano wa kuigwa kwa vijana
na wabunge wengine.
“sisi wazee
wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana limeridhishwa na uchapakazi wako kwani
maendeleo tunayaona kwa macho yetu,tulikuwa tunasikia tu katika mikoa mingine
kuwa kuna maendeleo lakini leo Ludewa kunafunguka kutokana na jitihada zako
hivyo tunatoa kiasi hiki kidogo ili kukuunga mkono katika kuliongoza jimbo la
Ludewa tunaomba uwaeleze na vijana wenzio wa wilaya hii wanao ishi mjini kurudi
na kufanya maendeleo nyumbani kama wewe”,alisema Mzee Mwanawalifa.
Mzee Mwanawalifa alisema kuwa wazee
wanasikitishwa sana na baadhi ya vijana waliolowea mijini bila kukumbuka
nyumbani na kuiendeleza miji yaw engine hali ambayo inakuwa mbaya wakati
wanapofariki na kurudishwa makwao kukiwa hali mbaya hivyo alimuomba
Filikunjombe kuwakumbusha vijana hao kurudi nyumbani na kufanya maendelo ili
kuikomboa wilaya ya Ludewa katika wimbi la umaskini.
Aidha katika
ziara hiyo ya kijiji cha Mbwila Filikunjombe aliweza kutoa bati miamoja katika
ujenzi wa nyumba ya Katekista katisa katoliki Mbwila na bati miamoja tena
katika ujenzi wa kanisa la Anglikana Mbwila hali ambayo imewafanya wananchi wa
kijiji hicho kushukuru pia kwa kuwaletea mradi wa maji.
Akitoa
hotuba yake Filikunjombe alisema kuwa kijiji hicho kina bahati ya kuwa na
maradi mkubwa wa maji lakini jitihada zinafanyika kuwaletea umeme wananchi wa
kijiji hicho ambao wanashauku kubwa ya kuwa na nishati hiyo ambayo imeshafika
katika kijiji cha jirani cha Luana.
Filikunjombe
aliwashukuru wazee wa Mbwila kwa kitendo cha kumchangia fedha za kuchukua fomu
ya kugombea ubunge kwa mara ya pili alisema kuwa anashukuru kwa kuona wananchi
wanatambua mchango wake wa maendeleo katika wilaya ya Ludewa kwani ni faraja
iliyoje unapoona wananchi wanatambua juhudi zako za kimaendeleo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment