WATU 26
wakazi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
wamehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kufanya maandamano kinyume
cha sheria, kulipa faini ya shilingi laki mbili kila mmoja kwa kosa la kupiga
mawe kitua cha polisi Mlangali na kuvunja madirisha na kosa la tatu kulipa
faini ya shilingi laki mbili kwa kosa la kupiga mawe gari la RCO Mkoa wa Njombe,
Akisoma
hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick
Lukuna alisema mbali na hukumu hiyo washtakiwa watatakiwa kulipa shilingi 48,470
kila mmoja kama fidia kwa ajili ya kufanya matengenezo kituo cha polisi pamoja
na kulifanyia matengenezo gari la RCO Mkoa wa Njombe.
Lukuna
alisema kuwa june 2 mwaka jana washtakiwa walivamia kituo cha polisi wakitaka
kukabidhiwa Askari aliyefahamika kwa jina la Kibasa ambaye alikuwa akifanya
mapenzi na masichana ambaye siku ya tukio aliondoka nyumbani kwao usiku n
akwenda kwa askari huyo na kumuacha mtoto mdogo na baadaye alifariki dunia kwa
kuungua na moto wa kibatari.
Awali
mwendesha mashtaka mratibu wa jeshi la polisi ambaye ni mkuu wa kituo cha
polisi Ludewa aliiomba mahakama kutoa adhabu kari kwa washtakiwa ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama zao za kujichukulia sheria mkononi
kwa sababu matukio ya kuvamia vituo vya polisi yameshamiri nchini na kutishia
amani.
Lukuna
aliongeza kuwa mshatakiwa atakayeshindwa kulipa faini na fidia hiyo atatakiwa
kutumikia jela miaka miwili,hata hivyo washtakiwa wengi walilipa faini na fidia
hiyo iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ludewa.
mwisho
No comments:
Post a Comment