Charles Keiya katibu tawala wilaya ya Ludewa
Fortunatus Fungatwende Katibu wa Mbunge wa Ludewa Deo Ngalawa
Diwani wa Mundindi Mh
Fortunatus Fungatwende akihutubia kata ya Nkomang'ombe
JAMII HURU NA MZEE WA NAKOZI
Wednesday, June 22, 2016
Saturday, April 23, 2016
Sunday, April 17, 2016
Kauli ya Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ya kuwataka vijana
kufanyakazi badala ya kuamka asubuhi na kuanza kunywa pombe au kucheza pool
sasa imeanza kueleweka miongoni mwa wananchi hata maeneo ya vijijini ambapo wamelipongeza
jeshi la polisi kwa kufanya msako kila siku asubuhi.
Wednesday, August 12, 2015
WATU 26 JELA KWA KUPIGA MAWE KITUO CHA POLISI NA KUHARIBU GARI LA RCO NJOMBE,
WATU 26
wakazi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
wamehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kufanya maandamano kinyume
cha sheria, kulipa faini ya shilingi laki mbili kila mmoja kwa kosa la kupiga
mawe kitua cha polisi Mlangali na kuvunja madirisha na kosa la tatu kulipa
faini ya shilingi laki mbili kwa kosa la kupiga mawe gari la RCO Mkoa wa Njombe,
Akisoma
hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick
Lukuna alisema mbali na hukumu hiyo washtakiwa watatakiwa kulipa shilingi 48,470
kila mmoja kama fidia kwa ajili ya kufanya matengenezo kituo cha polisi pamoja
na kulifanyia matengenezo gari la RCO Mkoa wa Njombe.
Lukuna
alisema kuwa june 2 mwaka jana washtakiwa walivamia kituo cha polisi wakitaka
kukabidhiwa Askari aliyefahamika kwa jina la Kibasa ambaye alikuwa akifanya
mapenzi na masichana ambaye siku ya tukio aliondoka nyumbani kwao usiku n
akwenda kwa askari huyo na kumuacha mtoto mdogo na baadaye alifariki dunia kwa
kuungua na moto wa kibatari.
Awali
mwendesha mashtaka mratibu wa jeshi la polisi ambaye ni mkuu wa kituo cha
polisi Ludewa aliiomba mahakama kutoa adhabu kari kwa washtakiwa ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama zao za kujichukulia sheria mkononi
kwa sababu matukio ya kuvamia vituo vya polisi yameshamiri nchini na kutishia
amani.
Lukuna
aliongeza kuwa mshatakiwa atakayeshindwa kulipa faini na fidia hiyo atatakiwa
kutumikia jela miaka miwili,hata hivyo washtakiwa wengi walilipa faini na fidia
hiyo iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ludewa.
mwisho
KWA WAPENDA ELIMU NDANI NA NJE YA WILAYA YA LUDEWA
Mfululizo wa
vitabu mbalimbali vinavyopatikana wilaya ya Ludewa ikiwa mwandishi wa vitabu
hivyo anapatikana Ludewa mjini katika mtaa wa Mkondachi.
Vitabu hivyo
vya hadithi na masomo ya Kiswahili unaweza kuvipata Ndanda Mission,Imiliwaha
mission Njombe na Ndumbi store Ludewa mjini katika stand ya mabasi.
Bei za vitabu hivi ni shilingi 2000 kwa Ludewa mjini lakini vimekuwa na bei tofauti katika maeneo mengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)