Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina ya Global Fund
na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza
kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini
Quebec, Canada
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi
wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano
wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec,
Canada
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura
kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa
kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)
ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia kura
agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda
iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya
Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto
kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe.
Hamad Rashid Mohamed
Spika
wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa
kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani
(IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila
anayehudhuria Mkutano huo pia.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokutana na
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili namna bora ya
kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka
ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama
kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo
Ujumbe
kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashid
na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada kuhusu “Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada
No comments:
Post a Comment