WAHAMIAJI haramu 100
kutoka nchi ya Ethiopia wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi kumi na
mbili(12) jela kwa kuingia nchini bila kibali wala paspoti.
Akisoma hukumu hiyo
jana hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa katika mkoa wa njombe
Fredrick Lukuna alisema kwa kuwa washtakiwa wamekiri kutenda kosa hilo mahakama
inawatia hatiani na watatumikia kifungo cha miezi kumi na mbili (12) jela.
Lukuna aliongeza kuwa
washtakiwa walitenda kosa hilo chini ya kifungu namba 31(1) na (2) cha sheria
ya uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995 na kwamba watatumikia kifungo hicho huku
wakisubiri taratibu za serikali kuwarejesha nchini kwao.
Awali akisoma hati ya
mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwendesha mashtaka wa idara ya uhamiaji aliiambia
mahakama kuwa Novemba 13 mwaka huu majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha
Ilela Manda tarafa ya mwambao wa ziwa nyasa bila halali na kwa makusudi
washtakiwa waliingia Jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kibali wala pasipoti.
Kabla ya kuhukumia
jela wahamiaji hao haramu walihukumiwa kulipa faini ya shilingi elfu kumi kila
mmoja(10,000) lakini wakashindwa na ndipo hakimu akawatia hatiani na kuamuru
kutumikia kifungo cha mwaka jela kila mmoja huku taratibu za kuwarejesha makwao
zikifanyika.
Katika kesi nyingine
mahakamani hapo kijana Richard Msemwa (17) mpangwa na mkulima wa kijiji cha
Luafyo juu Lugarawa amechapwa viboko 12 matakoni baada ya kupatikana na hatia
ya kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 jina tunalo chini ya kifungu 130.
Aidha kufuatia
maadhimisho ya kutimiza miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara wafungwa 6 wa makosa
mbalimbali katia gereza la Ibihi wilayani Ludewa wameachiwa huru na msamaha wa
rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Akizungumza na gazeti
hili mkuu wa gereza hilo kamishna msaidiza Mwaisabila wa jeshi la magereza
alisema wafungwa hao wameachiwa kwa mujibu wa sheria na kwamba hajapata pengo
lolote kufuatia kuachiwa kwa msamaha wafungwa hao.
Ni desturi kwa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwaachia wafungwa wa makosa madogomadogo kwa
msamaha Desemba 9 kila mwaka ili kwenda sambamba na sherehe za uhuru.
MWISHO
No comments:
Post a Comment