. Ni Baada ya shule
yao kupoteza mwelekeo
Na Bazil Makungu Ludewa
WAUMINI wa kanisa
la yesu kristu mkombozi parokia ya
Ludewa mjini jimbo katoliki la njombe wamegoma kuendelea kuchangia shule ya
sekondari ya st Alois inayomilikiwa na kanisa hilo kwa madai kuwa utawala
uliopo umepoteza mwelekeo.
Wakizungumza mbele ya
katibu wa elimu na malezi bora wa jimbo katoliki la njombe Fr Bruno Henjewele
waumini hao walisema tangu Askofu wao
Alfred Maluma amhamishe padre mchapakazi Dominic Mlowe ujenzi katika sekondari
hiyo umesimama kutokana na uzembe wa padre Ladislaus Mgaya.
Waliongeza kuwa kama shule
itaendelea kuwa chini ya meneja mpya padre Ladslaus Mgaya hawako tayari kutoa
michango na wananweka silaha chini kutokana na padre huyo kushindwa kuendesha
shule kwa kufuata mipanga na misingi mizuri alianzisha mwenzake Fr Dominic
Mlowe.
“” sisi hatuko tayari
kutoa wala kushiriki katika ujenzi kutokana na dharau iliyoneshwa na askofu kwa
kumhamisha padre mchapakazi Dominic ambaye kila muumini pamoja na wananchi
walimkubali na kujitolea kwa asilimia miamoja bila kusukumwa kama suala ni
maendeleo basi tunaomba fr Dominic arudishwe tuko tayari kuchangia.”” walisema waumini
hao walioneshwa kukerwa na usimamizi mbovu wa shule yao
Waumini pamoja na
mambo mengine wamemshutumu padre Mgaya kwa kukumbatia kila kitu yeye mwenyewe,
kushindwa kutoa taarifa ya maendeleo ya shule ikiwemo mapato na matumizi na
kutokuwepo uwazi, huku wengine wakitishia kuwahamisha watoto wao kama askofu
hatachukua hatua stahiki.
Awali akitoa taarifa ya
mradi wa ujenzi wa sekondari ya st alois kuanzia mei 2004 hadi Agost 31 2010
kwa katibu wa elimu na malezi jimbo Fr Bruno, mwenyekiti wa halmashauri ya
walei parokia hiyo mzee Linus Njala alisema hadi sasa fedha iliyotumika ni
m.637,693,415 ambapo jimbo limechangia sh m. 4.5 tu.
“’’’ kati ya fedha
hizo shilingi m. 520.9 zilitolewa na padre Dominic Mlowe mwanzilishi wa shule
hiyo ambaye hata hivyo alihamishwa ghafla julai 2010 huku waumini wakihitaji
mchango wake sana.
Hata hivyo baada ya
padre huyo kuhamishwa waumini wakaandika barua kumwomba askofu Alfred maluma kuruhusu
padre Dominic kuendelea na ufadhiri wa
shule hiyo akiwa katika parokia ya Kisinga hadi mradi wa ujenzi utakapokamilika
lakini Fr Mgaya na Askofu walipuuza maombi hayo na ndipo wakaamua kuacha
kuchangia shule hiyo.
Pamoja na shule hiyo
kuendeshwa vibaya huku kukiwa na migogoro ya kutokuelewana kati ya meneja na
mkuu wa shule na kwa upande mwingine walimu na meneja ndipo waumini wakataka
kujua nini nafasi ya parokia katika shule hiyo kwa sababu ni muda mrefu hakuna
taarifa ya mapato na matumizi kama ilivyokuwa awali.
Mzee Innocent Mbawala
akamwambia katibu wa elimu na malezi jumbo kuwa yeye mwenyewe na waumini wa
Ludewa wamekumbwa na kuharibika kwa uchumi kwenye familia zao kutokana na
kutumia muda mwingi kujitolea kwenye ujenzi wa shule hiyo halafu shuel haiendi
inauma sana.
‘’” padre huyu
ameshindwa kuendesha shule siyo kila padre anaweza utawala kila mmoja anayo
karama yake huyu ameshindwa ni vema kama kweli tunahitaji maendeleo ya shule
basi arudishwe Fr Dominic ndiyo hitaji la waumini””. Alisema Vivian Chiwango na shambamtwa
Mzee Gerordi Kayombo wakalalamikia
mfumo unaotumiwa na uongozi wa kanisa hilo wa kutoa maagizo kutoka juu huku
yakitekelezwa chini badala ya kuibuliwa na waumini wenyewe kwa manufaa yao.
Mambo yaliyopelekea
kuitishwa kikao hicho cha dharura ni pamoja na kutopata majibu sahihi na ya
kuridhisha kutoka kwa Fr Ladislaus Mgaya ambaye ndiye meneja wa shule
anayemwakilisha mmiliki Askofu wa jimbo.
Swali lililokuwa
likiwasumbua waumini hao ni juu ya nani mmiliki wa shule na faida ya wanaLudewa
lakini mkanganyo huo uliwekwa bayana na
katibu wa elimu na malezi jimbo na waumini kuonekana kuridhika na majibu ndipo changamoto
na lawama zote zikaelekezwa kwa Fr mgaya lakini katibu wa elimu jimbo
aliyapokea malalamiko na kuahidi kuyatendea kazi.
“”tatizo la umiliki wa shule kuwa mikononi mwa
askofu siyo tatizo tatizo letu ni mapato na meneja kushindwa kuendesha shule,
mambo hayaendi kabisa hapa, mamlaka yote amejilimbikia meneja na bila
kerekebisha uongozi hatuko tayari kushiriki kwa namna yoyote.’’’’ Alisema Gerordi Kayombo
Akitoa ufafanuzi Fr
Mligo alisema jimbo katoliki njombe linaundwa na wanafamilia wa njombe askofu
yeye ni kama kiranja katika miradi na shughuli zote za maendeleo huku
watekelezaji ni wa miradi wakiwa waumini wa Ludewa, Njombe, Makate,Wanging’ombe
na sehemu ndogo ya Kyela.
Kwa mujibu wa maelezo
ya padre aliyeongazana na msafara huo ambaye hakupenda jina lake liandikwe
alisema kila jambo lina mwisho na kuongeza kuwa padre Ladislaus Mgaya alikuwahi
kuwa katibu wa Askofu akatolewa badaye akapewa kuendesha hospitsri ya Lugarawa
mambo hayakwenda vizuri hatimaye akaletwa parokia ya Ludewa na waumini wanaonesha
kutomhitaji sasa hiyo nikazi ya Askofu kumrudisha fr Dominic au kumtuma
mwingine.
mwisho
No comments:
Post a Comment