Sunday, December 2, 2012

WHO YATOA SEMINA YA CHANJO



Na Lucy Mtitu Ludewa

Shirika la afya dunian (WHO) kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imeanzisha semina ya uchanjaji chanjo kwa watoto wenye umri chini ya mwaka  mmoja itakayoanza January 2013 kutokana na kuona vifo vya watoto wadogo vinazidi kuongezeka .

Hayo yalisemwa jana na mratibu wa afya mkoa Bi.Mariam Mohamed  katika semina ya uchanjaji chanjo kwa watoto wadogo na kasema kuwa wameamua kuanzisha kampeni ya uchanjaji chanjo ili kunusuru maisha ya watoto wadogo ambao kinga yao mwilini haiwezi kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Akifungua semina hiyo mganga mkuu wa wilaya Dr.Happines Ndoss aliyataja baadhi ya  magonjwa yatakayotolewa chanjo  kuanzia January 2013 kwa watoto hao ni pamoja na kifua kikuu, surua, kupooza, pepopunda, dondakoo, kuhara na nimonia.

Pia bw. Ndoss aliwataka wazazi wenye watoto wadogo kuhamasika kutokana na chanjo hiyo hasa kwa wale wanaotokea mbali na vituo vya afya kwa lengo la kuboresha afya ya mototo pasipo kutupilia mbali suala la usafi wa mazingira, kuwepo kwa vyoo na chakula safi.

Hata hivyo Bi.Mariam aliwataka wananchi kutambua chanjo hiyo haitawahusu watoto wenye umri zaid ya mwaka mmoja kwani kinga ya mototo mchanga ni ndogo ndomana inabidi watoto hao waanze kupatiwa chanjo wakiwa na wiki sita 6  na akifikia umri wa miezi 9 atapewa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa surua.

Kwaupande wake mganga mkuu wa wilaya Dr. Ndoss alizitaja changamoto zitakazowakumba kutokana na chanjo itakayoanza January 2013 ni pamoja na  baadhi ya wananchi na viongozi wa dini kutokuwa na uelewa juu ya chanjo hiyo pamoja na kukosa wasaidiz ambalo tatizo hilo lipo juu ya uwezo wao vituo vya afya wilayani humo kuwa vingi.

“wasaidizi wanahitajika 30 lakini waliopo hadi sasa hawazidi 8 na maafsa wakuu wapo 4 ni zoezi ambalo ni changamoto kubwa kwa idara ya afya kuweza kuweza kufanikisha zoezi zima la uchanjaji chanjo kwa watoto wadogo”Dr. Ndoss alisema”

Dr. Ndoss alionyesha mfano wa vichupa vya dawa ambavyo vinatumika kuhifadhia dawa ya chanjo ya kuhara ambayo inagharimu dola 35 yenye thamani y ash. 5600 kwa kila kityubu na wizara ya afya na ustawi wa jamii inahusika kupanga bajeti ya chanjo hiyo.

Naye mh. Diwani wa kata ya Ludewa bi. Monika Mchilo akizungumza katika semina alitilia mkazo zoezi la usafi kwa kuwataka viongozi wa afya wa wilaya ya ludewa kusimamia ipasavyo kabla zoezi la chanjo kwa watoto hao halijaanza kwani itasababisha magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu.

Zoezi hili la chanjo kwa watoto wadogo ni zoezi la kitaifa na kila mwananchi anahitajika kuwajibika kwani semina hii imefanyika katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata mkoa hadi kata.

MWISHO



No comments:

Post a Comment