Na Bazil Makungu
WANANCHI wa kata ya
Makonde mwambao wa ziwa nyasa wilayani Ludewa katika mkoa njombe wamemtaka mkuu wa mkoa wa njombe Kapteni
mstaafu Aseli Msangi kuondoka na diwani wa kata hiyo Cryspin Mwendakote
mwakasungura kwa kile walichodai ni fisadi.
Tukio hilo lilitokea
Novemba 26 mwaka huu majira ya mchana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha Makonde ambapo pamoja na mambo mengine mkuu wa mkoa wa njombe
alipita kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo katika tarafa ya mwambao wa
ziwa nyasa.
Hali ya sintofahamu
ilianza kujitokeza mapema baada ya mkuu wa mkoa na msafara wake kufika kijijini
hapo kwa usafiri wa boti ya halmashauri na kupokelewa na watu wachache huku
wengine wakijishughulisha na kuandika mabango yenye jumbe mbalimbali iliwemo
bango kubwa la kumtaka mkuu huyo kuondoka na diwani.
“” Tunashukuru kwa ujio
wako mkuu wa mkoa lakini tunaomba uondoke na diwani kwa kuwa tumechoshwa na
tabia yake ya ufisadi uliokithiri.”” Ilisema sehemu ya maneno katikamabango
hayo
Hata hivyo baada ya
mwenyekiti wa kijiji hicho kufungua mkutano wa hadhara hali ya hewa ilibadilika
wakati wa utambulisho ambapo miguno na dharau vilitawala mkutano na ndipo
mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha
akalazimika kusimama na kueleza utaratibu na sheria zinazolinda mkutano huo.
“” mkutano huu wa mkuu
wa mkoa upo halali na upo kwa mujibu wa sheria kwa hiyo mtu yeyote asijisahau
na kuleta mambo yasiyofaa na kama kuna yeyote mwenye shida atumie hekima na
busara kwa kutaka ufafanuzi, zaidi ya hapo hatutasita kuchukua hatua stahiki
kwa atakayekiuka.”” Alifoka Madaha
Kufuatia hali hiyo mkuu
wa mkoa kabla ya kuwaeleza wananchi mambo aliyotembelea akalazimika kutoa elimu
na ufafanuzi kwa wananchi hao kuhusu sheria na taratibu za kumwondo diwani
madarakani.
Msangi alisema njia ya
kwanza ya kumwondoa diwani ni kupeleka malalamiko mahakamani ambapo akipatikana
na hatia na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi mine akimaliza kutumia kwa
mujibu wa sheria atarudi kuendeleanaudiwani wake, lakini kifungo kuanzia miezi
na kuendelea udiwani wake utakuwa umekoma.
Njia ya pili mkuu huyo
akaitaja kuwa ni kwa kubiri amalize muda au kipindi chake cha miaka mitano
,nakumwondoa kwa njia ya kupiga kura baada ya uchaguzi kuitishwa na tume ya
taifa ya uchaguzi na njia ya mwisho ni diwani kufariki na tume ya uchaguzi
kulitangaza jimbo kuwa wazi.
Baada ya ufafanuzi huo
wananchi walibaki midomo wazi na ukimya kutawala mkutanoni hapo, jambo hili
likaonesha wazi kuwa walikosa elimu kuhusu ni sheria zipi zinazoweza kumwondoa
diwani wao madarakani lakini wakaanza kulaumiana wenyewe kuwa kuna watu
wanawaburuza kwa maslahi binafsi.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka
2010 wananchi wa kata ya makonde wameendelea kuendekeza na kuabudu makundi na
makovu ya uchaguzi yasiyo na msingi huku wakisahau kufanya hata shughuli za
maendeleo yao wenyewe.
Hii ni kutokana na
uelewa mdogo wa mambo kunakopelekea wajanja wachache kuwaburuza kwa maslahi
binafsi huku wao wakijivuta nyuma wakati wa ugeni au viongozi wa wilaya na mkoa
wanapokuja kutembelea kata hiyo.
Katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2010 diwani Crispin mwendakote mwakasungura alipata kura (400) mia nne
huku mpinzani wake kupitia chademaakiambulia kura (100) mia mojatu.
mwisho
No comments:
Post a Comment