Friday, January 18, 2013

DC ATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2005 HADI 2012.



                 Na Bazil Makungu Ludewa
MKUU wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Juma Madaha ametoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya nne ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuwataka wananchi wajiunge na saccos au vyama vya ushirika ili kujikwamua na umaskini wa kipato uliokithiri.

Akiwahutubia wananchi wa Ludewa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya mkuu huyo alisema wananchi wa Ludewa wameshiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi katika sekta za kilimo, ufugaji, upasuaji mbao, uvuvi, biashara, ajira za maofisini na viwandani ikiwemo kuimarishwa usimamizi na ufuatiliaji katika mamlaka za serikali za mitaa.

SEKTA YA KILIMO; katika kufanikisha mpango huu serikali imetoa ruzuku ya pembejeo za kilimo zenye thamani ya shilingi bilioni 7,065,796,000 kiasi hicho cha feha kimeweza kuwanufaisha wakulima kulima ekari 97,611 za mazao ya mpunga na mahindi.

Madaha akaongeza kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara umepanda na kufikia tani 43,644.9 kwa mwaka 2012 ukilinganishwa na tani 24,946.7 mwaka 2005 hii ni kutokana na uzalishaji tija kwa zao la mahindi kutoka tani 1.6 kwa hekta hadi kufikia tani 2.4 kwa hekta.

Zao la mpunga kutoka tani 2.7 kwa hektana kufikia tani 4.4 kwa hekta, ndizi kutoaka tani 10 kwa hekta hati wastani wa tani 14 kwa hekta na viazi mviringo kutoka tani 4.7 kwa hekta hadi tani 7.7 kwa hekta huku takwimu zikionesha kuwa mwaka 2011/12 wilaya ina ziada ya tani 91,234 za nafaka na tani 25,684  za viazi mviringo na mihogo.

Katika kuboresha, kuthibiti na na kufuatilia taarifa za fedha za umma katika taarifa yake mkuu wa wilaya akongeza kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kimepatiwa gari na kumputa ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji taarifa za ukaguzi kwa wakati.

‘’’’Ndugu wananchi Halmashauri imejengewa uwezo katika matumizi ya rasrimali watu na mali chini ya program ya shirika la tunajari nah ii imewezesha halmashauri kutoa huduma kwa viwango na imesaidia kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu na kuwa na sifa ya kuendelea kupata fedha za ruzuku za mamlaka za serikali za mitaa(Local Government Development Grant LGDG).’’’’ Aliongeza Madaha

SEKTA YA ELIMU;kiwango cha ufaulu kwa darasa la saba kimekuwa kikiongezeka na kupungua ambapo mwaka 2005 kiwango cha ufauru kilikuwa asilimia 68.6 na mwaka 2012 kiwango kimeshuka na kufikia asilimia 60.6 tofauti na lengo la wilaya ambalo ni asilimia 89 ifikapo mwaka 2015. 

‘’’’ ndugu wananchi serikali imeendelea kujenga na kupanua miundombinu kati shule za msingi kama nyumba za walimu na madarasa,mwaka 2005 kulikuwa na shule za msingi 98 lakini hadi sasa tunazo 102, madarasa yalikuwa 24 lakini kufikia 2012 yamefikia 46 nyumba za walimu zimeongezeka asilimia 66.6 kutoka nyumba 26 na kufikia 39 kwa 2012.’’’’ Akasema Madaha

Kwa upande wa shule za sekondari mwaka 2005 kulikuwa na shule 12 kati ya hizo mbili zikiwa za binafsi, lakini hadi kufikia 2012 kumekuwepo na shule 20 kati ya hizo 3 ni shule za binafsi ambapo mwaka 2005 wanafunzi walioingia kidato cha kwanza walifika asilimia 75.3 na mwaka 2013 wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza ni asilimia 100 ya wale waliofanya mtihani.

Nyumba za walimu wa sekondari zimeongezeka kutoka 39 zilizokuwepo 2005 hadi nyumba 89 zilizopo lengo likiwakufikia nyumba 293, kutoka madarasa 29 hadi 210 yaliyopo mwaka 2012, walimu wameongeka kwa asilimia 65.99 yaani kutoka walimu 84 waliokuwepo 2005 hadi 247 waliopo.

mwisho


No comments:

Post a Comment