Na Bazil Makungu Ludewa
NAFASI za Vijana
kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT) zilizotangazwa hivi karibuni zimeanza
kuingia dosari ambapo baadhi ya watendaji wengi nchini wanatumia matangazo hayo
kwa kujinufaisha kwa kuhongwa na watahiniwa ili wapate upendeleo.
Afisa
mtendaji wa kata ya Mlangali wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Edwardi
Makamba jana alibiruzwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Ludewa kwa
makosa mawili ikiwemo kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi laki moja kwa
njia ya M-PESA.
Akisoma hati
ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick
Lukuna, mwendesha mashtaka wa Takukuru Richardi Marekano akaiambia mahakama
kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya januari 3 na januari 10 mwaka huu.
Marekano
akaongeza kuwa mshtakiwa alitenda kosa la kushawishi na kasha kupokea mlungula
makosa yanayoanguki chini ya kifungu namba 15(1)a cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa no 11 ya mwaka 2007.
Awali
ilielezwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma aliomba fedha
za kitanzania shilingi laki tatu (300,000) kwa Nicodem Simoni Mtweve mkazi wa
mlangali kwa ajili ya kumpaupendeleo kwa kumpa nafasi ya kujiunga na jkt zoezi
linaloendelea hivi sasa nchi nzima.
Akizungumza
na gazeti hili Nico simoni mtweve alisema kuwa afisa mtendaji wa kata ya
Mlangali Edwardi Makamba alizoea kumwomba fedha ambapo hata mwakajana alimwomba
fedha akampa lakini hakufanikiwa kujiunga na jeshi nimechoka na wenzangu
wanisaidie. Aliongeza mtweve
Kesi hiyo
imeahirishwa hadi machi 4 mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa kwa kuwa upelelezi
ulikuwa bado kukamilika na mshtakiwa akapata dhamana kwa masharti ya mdhamini
mmoja mwenye mali isiyohamishika.
Aidha kesi
ya kuomba na kupokea rushwa inayomkabili mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Ludewa Matei felisian Kongo imeahirishwa hadi machi 4 mwaka huu itakapokuja kwa
mahakama kutoa maamuzi kama mshtakiwa anayokesi ya kujibu.
Awali kesi
hiyo iliahirishwa kwa upande wa utetezi kuomba mwenendo ili iweze kujibu hoja
zilizomo katika kesi hiyo kabla ya mahakama kuamua kama mshtakiwa anashtakala
kujibu hata hivyo baada ya majibizano pande zote zikaiacha mahakama uamuzi.
Katikakesi
hiyo mwenyekiti huyo anadaiwa kuomba rushwa kwa mlalamikaji ili aweze kumpa
upendeleo kwenye zabuni usambazaji vifaa vya komputa na tenda za ujenzi katika
halmashauri ya wilaya hiyo.
Wakati
huohuo kesi ya kushwishi na kutoa rushwa kwa ajili ya pembejeo inayomkabili
Afisa mtendaji kijiji cha Kipangala kata ya Luilo Yohana Pili na wenzake
imeahirishwa hadi machi 4 mwaka huu itakapo kujakwa kusikilizwa kufuatia
kukamilika kwa upelelezi wa kesi hiyo.
Akisoma kesi
hiyo wakati ikisikilizwakwa hatuaya awali mwendesha mashtaka wa takukuru
Richard marekano alisema upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na kwamba katika
kesi hiyo anatarajia kuleta mashahidi kumi na nane kwa upande wa mashtaka.
Inadaiwa
kuwa afisa mtendaji huyo alishirikiana na wakala wa pembejeo katika kijiji
hicho Sebastian Haule na mwenyekiti wa pembejeo Kilian Mbawala kuwashawishi
wananchi kusaini vocha hewa kasha kuwalipa kila mmoja shilingi 20,000 kinyume
cha sheria.
No comments:
Post a Comment