Friday, January 25, 2013

PAROKO AVAMIWA NA KUPORWA FEDHA ZAIDI YA M.3





         Na Bazil Makungu Ludewa

PAROKO wa parokia ya Mlangali Ludewa katika jimbo katoliki la Njombe Fr Volker (OSB) amevamiwa na majambazi nyumbani kwake na kuporwa pesa ya kitanzania jumla ya shilingi milioni 3 na dola 300.

Tukio hilo limetokea jana usiku wa januari 14 kuamkia 15 mwaka huu ambapo majambazi watatu wakiwa na bunduki moja na mapanga yaliingia kwenye mission ya kanisa hilo la Mlangali na kumfunga kwa kamba mlinzi na mpishi kabla ya kuingia katika sebule ya paroko huyo alipokuwa akipata chakula cha usiku.

Akizungumza na gazeti hili jana menyekiti wa balaza la walei katika parokia ya Mlangali mzee Mstaarabu Mtweve alisema yeye alipata taarifa za tukio hilo majira ya saa tano usiku na kwenda kushuhudia tukio hilo ambapo alimkuta paroko huyo akiwa analalamika kuumizwa miguu yote miwili.

“””” katika tukio hilo wezi walifanikiwa kuiba fedha taslimu milioni 3 ambazo aliziweka tayari kwa ajili ya kwenda kununua saruji kwenye duka la chapemba siku ya pili yake lakini watu hao wasio na huruma wamemfunga kamba paroko wangu mtu mzima na kupora fedha.’’’’’’ Alilalamika mzee Mstaarabu

Habari kutoka kwa wakazi wa kijiji cha mlangali zinasema kabla ya tukio kuna mtu alikwenda katika majengo ya parokia hiyo na pikipiki na kuzungumza na mlinzi na kasha kuondoka.

Muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini akaliambia gazeti kuwa paroko huyo na muda mfupi tu  tangu arudi likizo ya mwaka mmoja kutoka nchi kwao Ujerumani. 

‘’’’’ Fr Volker ni msaada sana kwa wana Ludewa kwani ameweza kujenga shule pekee ya kidato cha sita ya ulayasi kwa fedha zake mwenyewe hii ni mara ya pili kuibiwa fedha inauma sana’’’ alilalamika muumini 

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani alikiri kutokea na tukio hilo na kuongeza kuwa watu watatu wanashikiliwa kwa hatua za awali lakini juhudi zinaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo.

“”” ninavyozungumza hivi askari wangu chini ya mkuu wa upelelezi wilaya ya Ludewa Inspekta Peter Majengo wako katika eneo la tukio na tayari baadhi ya watuhumiwa wanahojiwa kuhusinana na tukio hilo.’’’’’ Alisema kamanda Ngonyani

Fr Volker (OSB) raia wa ujerumani hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa alikuwa amepelekwa katika hospitali ya mission ya Lugarawa  na Imiliwaha kuangalia hali yake ya kiafya.
 mwisho



 

No comments:

Post a Comment