Saturday, January 26, 2013

RUBADA YAKERWA NA UTITIRI WA MAGETI YA MAZAO NCHINI.


                Na Bazil Makungu Ludewa
MAMLAKA ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji(Rufiji Basin Development Authority(RUBADA) imeonesha kukerwa sana na uwingi wa mageti/vizuizi vilivyoenea nchi nzima kwa ajili ya kutoza ushuru wa mazao ya mashambani jambo linalowaongezea wakulima mzigo wa umaskini.
Akizungumza jana katika semina ya siku moja kwa madiwani na wakuu wa idara wa halmashauri ya Ludewa Mkoani Njombe Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo Aloyce Masanja alisema haoni sababu ya kuwa na utitiri wa mageti kama tuna nia ya dhati ya kuendeleza wakulima wetu.
Aliongeza kuwa nchi za ulaya wakulima wanaheshimika na wanatembea kifua mbele  kwa sababu wao ndiyo wenye fedha kuliko watumishi wa serikali, hii ni tofauti na Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika ambapo mkulima ndiye mtu fukara anayedharaulika kiasi cha kukosa hata  sifa ya kukopesheka.
’’’’Lengo la Rubada ni kuondoa vikwazo na kodi zisizo na tija kero na vizuizi katika kilimo, wakulima wanalima mazao kidogo lakini mageti na ushuru vyote ni mizigo mkulima wilaya moja ijakuwa na mageti zaidi ya kumi ya nini?.’’’’ Aliuliza Masanja
Masanja akaongeza kuwa serikali chini ya mamlaka ya uendelezaji wa mto Rufiji  Rubada imeanzisha program ya kuendeleza kilimo  katika ukanda wa kusini mwa Tanzania(SAGCOT) ambayo ni ubia kati ya sekta ya umma na binafsi wenye sura ya kimataifa ambao lengo lake ni kuleta mapinduzi katika kilimo kwa nia ya kuongeza uzalishaji wenye tija.
Aliongeza kuwa program hii  ilizinduliwa mei 2010 jijini Dar es salaam lengo likiwa kuchochea uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi ili kufanikisha ukuaji haraka wa kilimo endelevu na kuwepo kwa uhakika wa chakula, kupungua kwa hali ya umaskini na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Katika kuhakikisha vijana wanaokimbilia mjini wana rudi kuendesha maisha yao vijijini  Masanja alisema kuwa kuna haja ya kuanzisha makambi ya vijana kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha kubiashara ambacho ndiyo mtaji pekee wa kuondokana na umaskini wa kipato unaowakabili watanzania wengi.
Fidelis Lumato mkurugenzi wa halmashauri ya ya wilaya ya Ludewa akawataka wananchi kujiunga na vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali ikiwemo pembejeo ya ruzuku ili kujiongezea kipato na kuondokana umaskini.
Lumato aliwaambia wananchi kuwa moja ya lengo kuu la Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) ni kutoa fursa kwa wakulima wadogo ili waweze kulima kibiashara na kwa faida.
‘’’’’ Hii itawaunganisha na wakulima wakubwa ambao ni majirani zao pamoja na kunufaika huduma za uuzaji wa mazao katika eneo hilo na kuibua skimu ndogondogo za wakulima wanaozunguka mashamba makubwa ili wwaweze kupata faida ya upatikanaji pembejeo, huduma za ugani, kusindika mazao ili kuongeza thamani na urahisi wa masoko.’’’’ Alisisitiza Lumato
Upatikanaji wa mitaji kupitia sagcot utaambatishwa masharti nafuu na angalifu sana ambapo fedha zitatolewa kwa wawekezaji ambao wataahidi kuheshimu usawa na kujenga ubia endelevu kati yao na wazalishaji wadogo.
Tanzania ni nchi miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizosaini mkataba wa ushirikiano mpya katika masuala ya uhakika ya chakula na lishe na nchi nane tajiri sana duniani (G8) kwa lengo la kuhamasisha wafanyabiashara wa ndani na nje ili awwekeze katika kilimo.
               mwisho

No comments:

Post a Comment