Na Bazil Makungu Ludewa .
MZEE Leonadi Mhagama
Shetani (115) mkazi wa kijiji cha Ludende Ludewa katika mkoa wa Njombe jana
alitimiza ndoto yake ya kumwona mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na kusema
sasa mwenyezi mungu anaweza kumchukua katika dunia hii kwa sababu kiu yake ya
kumwona mbunge imetimia.
Shetani ambaye ni
muasisi wa chama cha mapinduzi(CCM)wilayani Ludewa amekuwa akikitumikia chama
hicho kwa muda mrefu na kushiriki katika kampeni za chaguzi mbalimbali lakini
kwa kuwa umri wake kuwa mkibwa amekuwa akishindwa kushiriki vikao vingi vya
chama na kushindwa kuonana na mbunge wa jimbo la Ludewa.
Katika hali isiyo
tarajia mzee Shetani aliwaambia wananchi waliokusanyika katika mkutano wa
hadhara kuwa amekuwa akisononeka moyoni mwake kiasi cha kufa huku akimwomba
mungu asimchukue kwanza mpaka atakapotimiza ndoto ya kuonana uso kwa uso na
mbunge na kumshika mkono.
Alisema alikua na
shauku ya kukutana uso kwa uso na mbunge huyo kijana kutokana na sifa anazozisikia
katika vyombo vya habari namna mbunge huyo anavyokemea uovu kwa nguvu zote bila
kuogopa vitisho vya wahujumu uchumi hao.
‘’’’’ nimekuwa
nikiumia moyoni ni lini nitamwona mbunge huyu na wakati Fulani nikiugua
nasononeka moyoni na kumuomba mungu asinichukue kwanza mpaka nipeane mkono na
mbunge wangu kwa sasa hata mungu akinichukua sina kinyongo maana ndoto yangu
imetimia.’’’’ Alisema kwa furaha mzee Shetani.
Filikunjombe alifika
katika kijiji cha Ludende na kupokelewa kwa kuvalisha shada la maua na mzee
shetani kama heshima ya mfalme kuwasili kijijini hapo kutokana na uchapakazi
wake uliotukuka wa kuwatumikia wananchi.
Mzee Shetani alimsihi
Filikunjombe kutokatishwa tamaa na watu wanaotaka kuliangamiza taofa kwa
kutowatendea haki wananchi kwani yeye na wazee wengine wako nyuma yake kukemea
tabia hizo.
Alisisitiza kuwa
Tanzania ni nchi nzuri na inayoaminika na mataifa mengine kutokana na heshima
ya muasisi wa nchi hii hayati Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere enzi za utawala
wake.
Hivyo hangependa kuona
chama alichokiacha muasisi wa taifa hili kinakuwa na viongozi wasio na uzalendo
wan chi yao kwa kufanya ubadhirifu unsolididimiza taifa katika wimbi la
umaskini badara ya kuwa na maendeleo tofauti na enzi zake.
Mzee Shetani alisema
ni lazima kuwepo na viongozi wanaoweza kuthubutu katika kukemea uovu ndani ya
chama na Serikali kama alivofanya hayati baba wa Taifa hili ili kuweka usawa wa
kimaisha kwa watanzania.
Aidha Bw.Filikunjombe
alisikiliza ushauri wa kada huyo na kuahidi kuutendea kazi kwa kutoteteleka katika
maamuzi yake dhidi ya wanaoihujumu Serikali kwa kujilimbikizia mali za
watanzania.
Filikunjombe alisema
Tanzania inapaswa kuwa na watu wazalendo kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa
hayati baba wa taifa na wazee wengine mfano wa mzee Shetani katika kutetea
maslahi ya wananchi zaidi.
Alisema ni lazima
viongozi wa sasa wawaenzi wazee hao wakati Taifa linapotaka maendeleo zaidi na
kukabiliana na changamoto za kidunia zilizopo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment