Wednesday, January 30, 2013

UJENZI WA VETA LUDEWA, TUKO TAYARI KUCHANGIA, WANANCHI




                  Na Bazil Makungu Ludewa

WANANCHI Wilayani Ludewakatika Mkoa wa Njombe,wameihakikishia  serikali  na kuitaka kuanza haraka taratibu za ujenzi wa chuo cha ufundi stadi(VETA) Wilayani humo kwa kuwa wao wako tayari kuchangia nguvu zao kwa kufyatua tofali, kukusanya mchanga, kuchimba msingi pamoja na mambo mengine yatakayohitaji nguvu zao.

Wananchi wa Ludewa waliweka bayana utayari huo jana katika kijiji cha  Shaurimoyo kata ya Lugarawa mbele ya Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya vyuo vya ufundi stadi nchini Bw Zebadiah Moshi alipokwenda kijijini hapo yeye mwenyewe kujionea na kukagua eneo na ardhi kitakapojengwa chuo hicho cha kihistoria katika wiklaya hiyo yenye utajiri wa madini ya makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha Liganga.

Akimkaribisha Mkurugenzi wa Veta Taifa na kutoa taarifa kwa niaba ya wananchi mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akamwondoa hofu na kusema serikali haina sababu tena ya kusita kujenga chuo katika wilaya ya Ludewa kwa sababu wananchi wako tayari kuipunguzia serikali gharama kwa kuchangia nguvu zao katika baadhi ya raslimali ya nguvu zao katika ujenzi huo.

Filikunjombe akasema kuwa wananchi wameridhia na kutoa ardhi nzuri yenye ukubwa wa hekta 30 sawa na ekari zaidi ya 70 kwa ajili ya chuo hicho na tayari Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa ktumia wataalamu wake imeshapima tayari eneo hilo kwa gharama zake.

Naye Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha katika mkutano huo wa hadhara akaihakikishia serikali kuwa eneo hilo ni salama na kuwataka wananchi wa Ludewa kuchangamkia ujenzi huo kwa sababu serikali imetambua umuhimu wake na ndiyo maana imeacha kujenga chuo hicho sehemu zingine nchini ikaona na kutoa kipaumbele katika wilaya yao
.
‘’’’’ katika migodi ya machimbo ya madini ya liganga na mchuchuma watu 5000 wanategemea wilayani Ludewa kama wafanyakazi katika migodi hiyo ambapo kati yao watu 1000 ni wageni kutoka nje ya nchi’’’ akataharisha madaha


Madaha akawataka wananchi wa Ludewa kutimiza wajibu wao katika ujenzi wa chuo hicho ambacho ni ukombozi mkubwa hasa kwa Vijana wanaohangaika kutafuta ajira na kukimbilia mjini.”” Mbali na Vijana kupata ajira lakini wananchi wajiandae kwa kilimo cha mbogamboga na matunda bila kusahau ufugaji kwani kwa kutumia fursa hiyo wataondokana na umaskini kwa sababu watapata soko kwa urahisi kutokana na uwingi wa watu watakaokuja kufanyakazi katika migodi.’’’’ Alifafanua na kusisitiza Madaha 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Fidelis Lumato alimhakikishia Mkurugenzi mkuu wa veta kwamba halmashauri yake iko tayari kutoa ushirikiano kwake ili kuhakikisha ujenzi wa chuo hicho unakamilika kwa wakati ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na ya haraka zaidi
.
“”” ndugu Mkurugenzi wa vyuo vya ufundi stadi mimi kama Mkurugenzi wa halmashauri hii tunakuahidi kutoa ushirikiano wa dhati na taasisi yako kwa mabo yote utakayohitaji kadri ya uwezo wetu na wala usisite kuja ofisini kuhitaji msaada pale utakapokuwa umekwama.’’ Akamwondoa hofu Lumato
Hata hivyo Mkurugenzi mkuu wa VETA nchini Zebadiah Moshi akawatoa hofu wananchi hao kwa kuahidi kuanza mchakato wa ujenzi wa chuo hicho Aprili mwaka huu katika kijiji cha Shaurimoyo na kwamba hadi kufikia mwezi juni mwakani baadhi ya masomo yawe yameanza kufundishwa katika chuo hicho.

Alisema chuo hicho kitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia darasa la saba, kumi mbili na kuendelea na kwamba hata hivyo watatakiwa Vijana kupelekwa chuoni Vijana wazawa kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuja kuwafundisha wenzao na kwamba kufanyahivyo ni kupunguza uhaba wa walimu unaoweza kujitokeza baadaye kwa walimu kukimbia mazingira.
                    mwisho

No comments:

Post a Comment