Na Bazil Makungu Iringa
MTOTO Fransis Mgogi mwenye umri wa miaka sita mkazi wa kijiji cha
Migoli katika Mkoa wa Iringa amejeruhiwa vibaya katika mkono wake wa kushoto na
punda aliyekuwa akizagaa mtaani na kuzua
hofu miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea
jana majira ya saa 12;30 katika kijiji hicho mtoto Fransis alipokuwa akicheza
na wenzake huku punda hao wakionekana kuzurura hovyo mtaani bila kuwa na mwenyewe ambapo punda huyo bila
huruma alimkamata motto huyo mkono wa kushoto kwa meno yake na kumning’iniza
juu na kisha kukimbia naye mpaka wananchi walipoanza kumkimbiza punda huyo kwa fimbo na hatimaye kumuachia
motto.
Baba wa mototo Ndg Franc Mgogi
akizungumza na muandishi kwamasikitiko makubwa alisema tukiohili nilaajabu
lakini anawasiwasi na haliya huyo Punda ingawa kunakawaida ya Punda
kuzagaa bila kujulikana mwenyenao nahuwezi muuliza mtu.
Muuguzi wa zamu katika kituo cha Afya cha Kope Hilda Mligo
aliyempokea motto huyo baada ya kujeruhiwa na punda, akiwa katika hatua ya
kumhudumia alilazimika kutumia mwanga hafifu wa taa kutokana na kukatika kwa
umeme tangu saa tisa alasili jambo lililompa shida sana mhudumu huyo kutokana
na giza nene lililokuwa limetanda katika chumba cha Upasuaji.
Ilimbidi muuguzi huyo kutumia taa ya
mionzi ya jua ambayo ilikuwa na mwangamdogosana akiombamsaada wa kumulikiwa
anapomsafisha eneolililo jeruhiwa akagunduo shimokubwa lililo tokana na jino la
Punda likionyesha Mfupa wa nyuma ya mkono juu ya Kiwiko.
Haliiliomfanya
muuguzi kumshauli Mzazi akisha mpatia sindano ya kinga inabidi amkimbize
mjini jambolililo Mshitua mzazihuyo alisikika akisema uwezowa kukodi Gari hana
itambidi alale apande Basi asubuhi kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Iringa
kwa matibabu zaidi.
Kwabahatimbaya mudawotehuo Dr wa
zamu alikuwa hajafika..
Akizungumza na muandishi Dada mmoja
Esta John mkazi wa kijiji Migoli alisema Pundahuyo kaisha fanya matukio zaidi
ya hilo alishamuuma mbwa na kuuwa kabisa siku za nyuma na janayake amemuuwa
Bata kwa kumkata shingo.
Juhudi za mwandishi kumpata Dr wa
mifugo kuthibitisha Uzima wa Punda huyo hazikufanikiwa pamoja na kupewa namba ya
Simu ambayo alipompigia haikupokelewa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment