Na Bazil Makungu,Ludewa.
Bank ya wananchi
Njombe(NJOCOBA)yenye makao yake mkuu mkoani Njombe imeamua kupanua huduma zake
kwa kufungua vituo vyake katika wilaya za Ludewa,Makete na mji wa Makambako ili
kuweza kuwafikishia huduma hiyo wateja wake.
Akizungumza jana wilayani
Ludewa Mkurugenzi mtendaji wa Bank hiyo Michael Ngwira aliitaka Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa kutenga fedha kwa ajili ya kununua hisa katika benki hiyo ya
wananchi na kuwahamasisha watumishi na wananchi kununua hisa ili kukidhi vigezo
vya kufungua kituo cha kutolea huduma za kibenki.
Ngwira pamoja na
wataalamu wengine walitembelea wateja wa banki ya Njokoba katika wilaya ya
Ludewa wakiwa na lengo la kutoa ufafanuzi kuhusiana na masula ya mikopo na
manufaa ya saccos katika kupitia benki hiyo.
“”” benki ya Njocoba
ya mjini njombe ni mali ya wananchi wa wilaya zote za mkoa wa Njombe hivyo ni
fulsa pekee kwa wananchi hao kunufaika nayo kwa kupata mikopo midogo midogo
itakayowawezesha kufungua biashara za kuwasaidia kuondokana na umaskini.”””
Alisema Ngwira
Naye afisa mikopo wa
Njocoba Danford Mfikwa akawataka wateja wake kuwa na subira kwani vituo hivyo
vinatarajia kuanza rasmi juni mwaka huu ili kwenda sambamba na changamoto
zinazowakabili wananchi hasa wajasliamali wadogowadogo wasiokopesheka na
makampuni mengine nao waweze kukopa na kujiendesha kimaisha.
Bw.Mfikwa alisema
bank hiyo pia hutoa huduma za mikopo ya pembejeo kwa wateja wake pindi
wanapohitaji mikopo hiyo hivyo ni fulsa pekee kwa wateja wakulima kuchangamkia
mikopo hiyo.
Aliwataka wakulima wa
wilaya ya Ludewa na makete kujiunga na saccos mbalimbali ili waweze kukopesheka
kwani wakulima wa wilaya ya Njombe wameweza kunufaika na bank hiyo kupitia
vikundi vya kuweka na kukopa.
Nao washiriki wa
warsha hiyo wilayani Ludewa walifurahishwa na kuunga mkono jitihada za benki ya
Njocoba na kwamba wamechoshwa na usumbufu wa kutumia benki moja na kuomba
uongozi huo kufanya haraka kufungua tawi kwani wako tayari.
Katika ziara hiyo mkurugenzi wa njocoba
alifanikiwa kuzungumza na kikundi cha Rafiki ambacho kinataria kusajiriwa hivi
karibuni na kuwa mwanachama wa Njocoba.
Aidha Bw.Ngwira
aliwataka viongozi wa kikundi cha Rafiki kuutangazia umma ili wananchi wengi
waweze kujiunga na kikundi hicho kitakachoweza kupata mikopo kutoka bank
mbalimbali.
SEKONDARI IKOVO
YAKOSA VYOO WANAFUNZI, WALIMU WAJISITIRI POLINI.
Na Bazil Makungu,Ludewa.
WALIMU na Wanafunzi
wa shule ya sekondari Ikovo iliyoko kata ya Ludende wilayani Ludewa katika mkoa
wa Njombe wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na shule hiyo
kukosa vyoo na maji zaidi ya miezi sita sasa.
Aidha zaidi ya walimu
13 na wanafunzi 200 wanalazimika
kujisaidia polini kutokana na shule hiyo kutokuwa na vyoo kwa muda mrefu kwa
kile kinachodaiwa halmashauri ya wilaya kuitelekeza shule kwa muda mrefu na
kupelekea shule hiyo kukumbwa na tatizo kubwa la kutokuwa na vyoo kwa wanafunzi.
Akizungumza na gazeti
hili afisa Mkaguzi wa shule wilayani Ludewa Florian Mvanginyi alikiri kufanya
ukaguzi shuleni hapo na kusema kimsingi shule ya sekondari Ikovo kwa sasa haina
sifa ya kuendelea kutoa huduma kwa sababu ni chafu haifai na pia mazingira ya
shule hatakiwi kuishi binadamu.
“” tumetoa maelekezo
kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa, uongozi wa shule na Kata ya
Ludende ilipo sule hiyo kuwa ofisi ya ukaguzi itafunga shule hiyo ifikapo Aprili
12 mwaka huu kama vyoo vitakuwa havijakamilika kwa sababu kuiacha shule na
wanafunzi kuendelea kuwepo shuleni hapo ni hatari sana kwa afya zao.”””
Alisisitiza Mvanginyi
Mvanginyi uhitaji wa
vyoo kataika shule hiyo ni 12 ya vyoo
ambapo kati ya hayo matundu saba ni kwa ajili ya wasichana, matundu matatu kwa
ajili ya wanafunzi wa kiume wakati matundu mawili ni kwa ajili ya walimu wa
shule hiyo.
Akazitaja changamoto
zingine zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa maji na nyumba za
walimu ambapo shule hiyo ina jumla ya walimu 13 lakini shule ina nyumba 6 kwa
hiyo walimu wanalazimika kuishi zaidi ya wawili katika nyumba moja.
Naye Makamu wa Mkuu
wa shule hiyo mwalimu Simoni Mwangalo Akizungumza jana alisema tatizo hilo lilisha wasilishwa katika
ngazi ya wilaya lakini hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa ili kuwanusuru
wanafunzi hao.
Mwalimu Mwangalo
alisema kuwa shule hiyo ambayo iliyoanzishwa mwaka 2007 imekumbwa na changamoto
nyingi zikiwemo za ukosefu wa matundu ya vyoo,ukosefu wa maji safi na salama na
kutokuwa na nyumba za walimu ambapo mpaka sasa shule hiyo ina jumlaya nyumba za
walimu tatu ambazo wanaishi walimu 13.
Hata hivyo wanafunzi
wa kike katika shule ya sekondari Ikovo wanaoishi hostel wanalazimika kulala
chini kutokana na ukosefu wa vitanda 48 shuleni hapo jambo linalohatarisha usalama wa wa afya za
wananfunzi shuleni hapo.
mwisho
No comments:
Post a Comment