DC LUDEWA AWATAKA
WANAWAKE KUWAKATAA WANAUME WASIOFANYIWA TOHARA
Na Bazil Makungu Ludewa
WANAWAKE Wilayani Ludewa
katika Mkoa wa Njombe wametakiwa kugoma
kwa kukataa kufanya mapenzi na wanaume wasiofanyiwa tohara kama njia mojawapo
ya ushiriki wao katika kampeni ya kupambana na kasi ya maambukizi ya virusi vya
ukimwi wilayani humo.
Akizungumza jana Mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha alisema wanawake wakiungana pamoja na kuamua
kuwakataa wanaume wanaokwepa tohara watakuwa wamesaidia kwa asilimia 60
kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe.
Madaha akaongeza kuwa
suala la ukimwi limekuwa likipigiwa kelele kila kukicha kwa njia mbalimbali
ikiwemo warsha, semina, makongamano na katika nyumba za ibada lakini lakini
kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ndiyo yanazidi kuongezeka kila siku
pengine ni kutokana na baadhi ya wanawake kutokuwa makini katika tendo la
kujamiiana.
“” ninyi wanawake
kataeni kabisa kufanya mapenzi na wanaume hao na wala msiwaonee aibu akina baba
wanaokwepa kufanyiwa tohara kwa kisingizio cha mila kwani mkifanya hivyo
mtakuwa mmelisaidia Taifa kupunguza kasi iliyopo sasa. ‘’’’ akasisitiza Madaha
Madaha alifikia hatua
hiyo kutokana na takwimu kuonesha kuwa wilaya yake ndiyo inayosadikika kuongoza
kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ikilinganishwa
na wilaya zingine zinazounda mkoa wa Njombe ambazo ni Makete, Njombe na
Wanging’ombe.
Alisema mila na
desturi ni tunu muhimu katika kuhakikisha uhai na ustawi wa jamii zetu lakini
kuna haja ya kuzichambua mila na desturi na kuziendeleza zilizo nzuri na
kuzikomesha zilizo mbaya zenye sura ya ukandamizaji, unyanyasaji, vitendo vya
ukeketaji, ndoa zisizo rasmi, ubaguzi wa kijinsia na kurithi wajane.
Aidha Madaha
alizitaja desturi nzuri kuwa ni pamoja na kuhimiza umuhimu wa kutekeleza tohara
kwa watoto wa kiume na wanaume kwa kufanya hivyo tutapunguza kasi ya maambukisi
ya virusi vya ukimwi na ukimwi katika jamii.
Kila jamii na familia
ihakikishe inawatahadharisha watoto juu ya namna bora ya kujenga mienendo
mizuri katika kusisitiza tabia njema zinazoendana na maadili na utamaduni wa
mtanzania na kuepusha watoto juu ya kasumba ya kuiga mienendo ya michafu ya
kimagharibi isiyo na tija kwa Taifa letu.
Mathalani mavazi na
mitindo ya uvaaji usio na staha wala adabu, tabia na mienendo tete isiyoleta
mantiki katika akili na zenye kupingana na maadili pamoja na mafundisho ya dini
zetu kama vile ngono, mapenzi na ndoa za jinsia moja.
No comments:
Post a Comment