.Mbunge aingilia kati na kuwapelekea
wananchi
Na Bazil Makungu Ludewa
DIWANI wa Kata ya
Masasi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Laurance Mahundi amelalamikiwa na
wananchi wake kwa kuzuia tanki la maji walilopewa na mbunge wao na kisha
kulitelekeza katika yadi ya ujenzi tangu mwezi februari mwaka huu huku
akishinda kucheza bao mjini wakati wananchi wakiteseka na maji.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti na gazeti hili wananchi wa kata ya Masasi walisema Julai 18
mwaka 2011 mbunge wao Deo Filikunjombe alifika katika kata yao kwania ya
kuwashukuru na ndipo wakamweleza shida wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa
maji unaosababishwa na ukosefu Tanki la kutunzia maji.
””” sisi wananchi wa
kata ya masasi tunatumia maji yaliyopo katika mtandao wa maji ya mchuchuma
manda na mabomba yakitoboka na maji kuanza kupotea huwa tunapata shida sana
lakini kama tungekuwa na Tanki la kuhifadhia maji tusingekuwa na shida ya maji.
Alisema kiongozi wa ngazi ya kata ambaye hakupenda jina lake liandikwe
Stanley Gowele ni
katibu wa mbunge wa Ludewa kwa upande wake alikiri kuwa wananchi wa masasi
walimwomba mbunge awasaidie tanki la maji kwa ajili ya kuhifadhi maji kutokana
na mabomba kutoboka kila wakati huku wao wakikumbwa na adha ya maji na
kulazimika kunywa maji yasiyosalama.
Gowele akaongeza kuwa
disemba 2012 mbunge alipata Tanki Dar es salaam na kulituma hadi Njombe na
februari mwaka huu alikodi gari kwa ajili ya kulipeleka tanki hilo hadi kata ya
masasi lakini diwani akataka lishushwe mjini Ludewa atalipeleka yeye.
,,,, Februari mwaka
huu mimi nilikodi gari kwa ajili ya kulisafirisha tanki la maji kutoka njombe
hadi kata ya masasi lakini nilipompigia simu diwani alipokee akajibu kuwa yeye
yuko safari na kuagiza lisipelekwe bila yeye hivyo lishushwe atalipeleka kwa
gari la halmashauri ndiyo lipo mpaka sasa.’’’’ Akasikitika sana Gowele
Alipoulizwa kwanini
alizuia tanki hilo lisipekwe na kwa nini hajapeleka hadi sasa diwani Mahundi
alijibu kwa kebehi kuwa siyo kazi ya mbunge kupeleka tanki katika kata yake na
kwamba atalipeleka muda ukifika bila kutaja na muda gani aliopanga kupeleka
tanki kwa wananchi walioliomba.
Naye kaimu mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Gladness Mwano alisema kuwa hana taarifa kuhusu
kucheleweshwa kwa tanki hilo lakini akaahidi kufuatilia taarifa hizo kwa
mhandisi wa maji wilaya ili kujua kwanini tanki limeendelea kuwepo badala ya
kuwapelekea wananchi mali yao
Masasi ni kata
inayokabiliwa na uhaba wa maji kutokana na kuwa na miundombinu isiyo ya
uhakika. Hata hivyo katibu wa mbunge wa Ludewa Stanley Gowele aliahidi
kulipeleka tanki la maji haraka ili kuwanusuru wananchi hao.
mwisho
No comments:
Post a Comment