NMB
LUDEWA YAWATAKA WATEJA KUTUNZA SIRI NA TAARIFA ZA AKAUNTI ZAO.
Na
Bazil Makungu
BENKI
ya NMB tawi la Ludewa katika mkoa wa Njombe imewataka wateja wake
kutunza taarifa na siri za akaunti zao ili kuepusha usumbufu kwa
benki hiyo na wizi wa fedha unaoweza kuwakumba wateja hao.
Akiongea
na waandishi wa habari jana meneja wa bank ya NMB lawi la Ludewa
Bw.Maulid Abdalah Mwingira alisema kumekuwa na wateja ambao hawana
siri juu ya taarifa zao za kibenk hali ambayo inasababisha wateja hao
kuibiwa fedha zao na kuilaumu bank wakati kosa liko kwa wateja hao.
Alisema
baadhi ya wateja wamekuwa wakiwaamini sana watoto na jamaa na
marafiki zao na kuwapatia namba za siri za account zao na baadae
kuibiwa fedha bila kujitambua na kupelekea kuilaumu bank bila msingi
wowote.
“napenda
kuweleza wateja wetu kuwa wasipende kutoa taarifa zao za kibenk kwa
kila mtu kwani wanaweza kuibiwa fedha zao na watu wanaowaamini,na
watambue kuwa kupitia mitandao ya simu mtu anaweza kuhamisha fedha
kutokana na wewe kumpa taarifa zao za kibenk”,alisema Bw.Mwingira.
Bw.Mwingira
alisema Bank hiyo ina wateja wengi sana nchini na kama kila mteja
atakuwa na tabia ya kutunza taarifa zake vizuri basi hakuna mtu
mwingine atakayeweza kuiba fedha katika account ya mwingine lakini
kama mteja mwenyewe hatakuwa na siri katika taarifa zake basi
ataruhusu kuingiliwa.
Aidha
aliwataka wanaoibiwa kwa uzembe wao wenyewe wasiwe na kauli ya
kuichafua bank hiyo kwani wafanyakazi wa bank ya NMB Tanzania ni
waadirifu na wako makini na kazi wanazozifanya na si vinginevyo
Kuhusiana
na Mitandao ya simu kuathiri huduma za kibenk Bw.Mwingira alisema
hakuna athari yoyote ya mitandao hiyo katika shughuri za kibenk
kutokana na mahusiano mazuri ya mitandao hiyo na Bank.
Alisema
kupitia mitandao ya simu wateja wa bank wanaweza kuweka na kutoa
fedha bila ya kufika bank hali ambayo imewarahisishia wafanyakazi wa
bank kutokuwa na mzigo mkubwa na kuweza kukusanya marejesho ya mikopo
kwa kutumia mitandao hiyo.
Bw.Mwingira
alisema kila kitu kina faida na hasara ndivyo ilivyo mitandao ya simu
katika huduma za kibenk kwani kuna watu ambao pia hutumia mitandao
hiyo katika wizi wa fedha nchini kwa baadhi ya bank.
Hali
ambayo inawafanya wafanyakazi wa bank kuwa makini na kazi yao na
katika kufuatilia account zote ili kubaini kama kuna wizi unaoweza
kujitokeza kwa kutumia mitandao hiyo na waliobainika kutumia vibaya
mitandao ya simu wameshachukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha
wimbi la wizi wa mitandao.
Bw.Mwingira
aliwataka wateja kuwa waangarifu na taarifa zao pia kuuliza kwa
wafanyakazi wa bank hiyo pale wanapoona kunautata ama hawajaelewa na
si kulaumu kwa vitu wasivyovifahamu,ili kupata ufumbuzi mapema
iwezekanavyo.
Mwisho.
DEREVA AFUNGWA JELA NA KUFUNGIWA LESENI
MAISHA
Na
Bazil Makungu Ludewa
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda jela
miezi kumi na mbili na kunywang’anywa leseni ya udereva na kisha
kufungiwa kutoendesha gari lolote katika maisha yake Edward Mliwa kwa
kusababisha majeraha kwa watu watano baada ya kupata ajali kwa
uzembe.
Akisoma
hukumu hiyo iliyochukua takribani masaa mawili hakimu mkazi mfawidhi
wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna alisema kuwa mahakama
yake imeridhika na ushahidi ulioletwa mbele yake na upande wa
mashtaka na kwamba mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi kumi na
mbili jela au kulipa faini ya sh hamsini elfu (50,000) kwa kila kosa.
Lukuna
mshtakiwa Edward Mliwa anashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo
kuendesha chombo cha moto kwenye barabara ya umma kwa uzembe na
kusababisha ajali iliyowajeruhi watu watano kinyume na sheria chini
ya kifungu 41, 50 na 63(2) cha sheria barabarani sura ya 168.
Hakimu
mkazi mfawidhi akaendelea kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba
12 mwaka 2012 katika kijiji cha Masasi barabara ya Ludewa Manda
wilayani Ludewa ambapo alikuwa akiendesha gari aina ya center yenye
namba za usajiri T 715 AZU akiwa amebeba abiria kupita kiasi.
Awali
mshtakiwa alikiri kosa moja tu ambalo ni kusababisha majeraha kwa
abiria watano lakini akakana kuhusika na kosa na uzembe akiwa na
chombo cha moto hata hivyo mahakama hiyo imeiamuru mamlaka ya mapato
nchini TRA kuifungia leseni ya mshtakiwa maisha kutokana na makosa
hayo.
Akiomboleza
mahakani hapo Edward Mliwa akaiomba mahakama kumwonea huruma na
kumpunguzia adhabu kwa sababu anayofamilia inayomtegemea, hata hivyo
alilipa faini na kupona kwenda jela.
No comments:
Post a Comment