Na
Bazil Makungu Ludewa
TAASISI
ya kuzuia na kupambana rushwa wilayani Ludewa (Takukuru) imempandisha
kizimbani mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
Atanasio Munge kwa makosa ya ubadhilifu wa jumla ya shilingi 4.2
milioni mali ya halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbele
ya hakimu mkazi mheshimiwa JUMA HASSANI wa katika mahakama ya mkoa
Iringa mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
Imani Mitume akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa anakabililiwa na
makosa manne ikiwemo matumizi ya nyaraka kosa linaloangukia kwenye
kifungu namba 22 ya sheria ya kuzuiaz na kupambana na rushwa namba
11/2007.
Makosa
mengine ni ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma chini ya namba
28(2) sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na 11 ya mwaka 2007,
kosa lingine ni kuibabishia hasara serikali shilingi milioni 4
makosa chini ya kifungu namba 10(1) jedwari la 57(1) na jedwari la
60(2).
Pamoja
na mhandisi Atanasio Munge mshtakiwa wa pili ni mfanyabiashara wa
mgahawa Videa Kayombo maarufu kama (mama hadija) ambaye jina,saini na
mgahawa wake vilitumika kutoa stakadhi zinazoonesha kuwa alitoa
huduma hewa ya chakula chenye thamani ya shilingi m.4.2 kwa wananchi
wa vijijini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji wilayani
Ludewa inayofadhiriwa na Benki ya dunia.
Akisoma
hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa (TAKUKURU) Imani Mitume alisema watuhumiwa wote wawili
walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2010 na 2012 na kwamba Vedea
Kayombo alitoa risiti za uongo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la
jinai.
Kufuatia
tukio hilo Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
Edings Mwakambonja ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kutoa
ushirikiano na ofisi yake kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
lakini pia akawahimiza kusimamia miradi inayopelekwa na serikali
katika maeneo yao.
Mwakambonja
pia amewataka watumishi wa umma kuwa waadlilifu katika kazi zao ili
kuiepushia serikali hasara na kusababisha kuzorota kwa huduma bora za
kijamii jambo linalosababishwa na watumishi wasio na uzalendo na nchi
yao.
mwisho
No comments:
Post a Comment